Monday, January 10, 2011

Ni hayo yali yo jili

wa 3-0 dhidi ya Uturuki huko Berlin na Urusi ilipata mshimshike huko Dublin, Republic of Ireland na hatimaye kushinda 3-2.
Ureno, iliyokuwa ikisuasua, ilizinduka na kuichapa Timu ngumu Denmark mabao 3-1 na Spain iliichapa Lithuania 3-1 ugenini.
Katika mechi ya Germany, Miroslav Klose aliifungia Germany mabao mawili na Mesut Oezil alifunga bao moja lakini hakushangilia bao hilo hata chembe kwani Uturuki ndiko wanakotoka Wazazi wake.
Belgium iliishinda Kazakhstan mabao mawili ugenini na bao zote zilipachikwa na Ogunjimi ambae awali aliamua kuichezea Nigeria anakotoka Baba yake lakini baadae akageuza mawazo na kuichezea Belgium alikozaliwa.
Katika mechi ya Ureno na Denmark, Nani wa Manchester United alifunga bao mbili ndani ya dakika mbili kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili Beki wa Ureno, Ricardo Carvalho, alijifunga mwenyewe na kuifanya mechi iwe 2-1.
Ronaldo aliwakikishia Ureno ushindi alipofunga bao la 3 dakika ya 85 na kuifanya Denmark ilale 3-1.
Katika Kundi C, Ireland ya Kaskazini ikicheza nyumbani Mjini Belfast iliibana mbavu Italy na kwenda nao sare 0-0.
Mabingwa wa Dunia, Spain, wakiwa ugenini, waliichapa Lithuania 3-1 kwa mabao mawili ya Fernando Llorente na David Silva.
Boa la Lithuania lilifungwa na Davydas Sernas.
Leo, kutakuwa na mechi mbili, France v Romania na Israel v Croatia.
Jumanne kutakuwa na lundo la mechi za Euro 2012 ikiwemo ile ya England v Montenegro