Wednesday, September 30, 2009

BIG BROTHER AFRICA REVOLUTION - Daily Updates - Day 23 (September 29, 2009)

Day 23 of M-Net’s BIG BROTHER REVOLUTION was filled with confrontation, romance – and sheep! On Sunday, Paloma told Itai that she felt betrayed by him when he didn’t keep his word. The next day, Itai told Big Brother that he was struggling with the tension in the house caused by the immorality that surrounds alliances. He felt like his alliance with the girls had no loyalty and wasn't sure who to trust.After his attempts to make amends with Paloma failed on Monday, he finally made his decision about who he is going to support and nominated Paloma and Liz. On Tuesday morning, Itai re-iterated his loyalty to Yacob and the twins, claiming that it is not about the money for him, but rather about true friendship. The drama continues!The housemates were handed their task on Tuesday, one which will surely push their endurance to the limit. Without knowing it, their task had actually started as soon as they woke up on Tuesday and will continue until they end their presentation on Thursday evening. Although the task has numerous components, the challenge is to not fall asleep during Big Brother's "waking hours". Big Brother decided that all housemates may sleep for a maximum of 4 hours on Tuesday night and 5 hours on Wednesday night

Manchester United v VfB Wolfsburg


Ndani ya Old Trafforf jijini Manchester, Mashetani Wekundu Man U watakwaana na Mabingwa wa Ujerumani Wolfsburg katika mechi ya pili ya Kundi lao kuwania Kombe la UEFA Champions LEAGUE.
Mechi nyingine ya leo kwenye Kundi hili ni kati ya CSKA Moscow v Besiktas.
Man U ilishinda mechi yake ya kwanza Kundini kwa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Besiktas na Wolfsburg, ikiwa nyumbani, iliibamiza CSKA Moscow 3-1.
Man U leo huenda ikaikosa nguvu kazi ya Winga Park Ji-sung ambae ni mgonjwa na pia upo wasiwasi kuhusu Michael Owen ambae ana tatizo dogo pajani.
Kipa Veterani Edwin van der Sar ameshapona na ameanza mazoezi lakini inaaminika leo Ben Foster ataendelea kuwa golini kwani van der Sar hajapata mazoezi ya kutosha.
Wolfsburg huenda wakamkosa Nahodha wao Josue mwenye matatizo ya goti ambalo alifanyiwa operesheni hivi karibuni.
Hata hivyo, nguvu ya Wolfsburg ni Mshambuliaji hatari toka Brazil Grafite na mwingine kutoka Bosnia, Edin Dzeko, Wachezaji ambao hupewa sapoti kubwa na mwenzao kutoka Bosnia pia aitwae Zvjezdan Misimovic.

LEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE


Apoel Nicosia v Chelsea
Leo saa 3 dakika 45 usiku, saa za bongo, Chelsea wanashuka Uwanja wa GSP Nicosia uliopo mjini Nicosia, Visiwani Cyprus, kucheza na Wenyeji wao Apoel Nicosia katika mechi ya pili Kundini mwao katika kinyang’anyiro cha UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Chelsea watashuka dimbani bila Nyota wao Michael Ballack, John Mikel Obi na Ashley Cole ambao ni majeruhi pamoja na Didier Drogba na Jose Bosingwa ambao bado wako kifungoni.
Ingawa Apoel Nicosia hawapewi nafasi kubwa kwenye mechi hii, Kocha wao Ivan Jovanovic anaamini wanaweza kufanya vizuri hasa baada ya kucheza vizuri katika mechi ya kwanza walipokuwa ugenini huko Spain na kutoka suluhu na Atletico Madrid.
Chelsea waliifunga FC Porto ya Ureno bao 1-0 katika mechi ya awali ya Kundi hili.
Mechi nyingine kwenye Kundi hili ni FC Porto v Atletico Madrid.

Monday, September 28, 2009

LEO MAN CITY v WEST HAM!!!!

Gianfranco Zola: "Bellamy alinifanya niwe Meneja Bora!!"

Meneja wa West Ham ambae aliwahi kuwa Staa wa Chelsea, Gianfranco Zola, amepasua kuwa Mchezaji mkorofi sana Craig Bellamy ambae sasa yuko Manchester City alimpa wakati mgumu alipokuwa West Ham na kumfanya yeye aongezeke uzoefu wa kuwa Meneja Bora.Bellamy, Raia wa Wales, aliihama West Ham Januari mwaka huu na kujiunga na Manchester City.Bellamy alipokuwa Liverpool ilibidi aihame Timu hiyo baada ya kudaiwa kumpiga na gongo la kuchezea Gofu mchezaji mwenzake John Riise na ashawahi kufarakana na Alan Shearer alipokuwa Newcastle.Wiki moja iliyopita Bellamy alitawala vichwa vya habari Magazetini baada ya kumzaba kibao shabiki alievamia Uwanja wa Old Trafford baada ya mechi kati ya Man U na Man City kumalizika kwa ushindi wa 4-3 kwa Man U.FA, Chama cha Soka cha England, kimempa onyo kali Bellamy kwa kitendo hicho.Na leo usiku, Timu ya Craig Bellamy, Manchester City, itapambana na Klabu yake ya zamani, West Ham na Meneja wa West Ham, Gianfranco Zola ametamka: "Nilipenda kufanya nae kazi! Ni kitu kigumu kwani ni mtu mwenye munkari! Lakini ukimchukulia kwa njia ipasayo ni Mchezaji anaekulipa kwa juhudi zake uwanjani!"Zola ameendelea: "Amenipa uzoefu na manufaa katika kazi ya Umeneja!"


Ebanaeee!!!! John Terry awakandya wenzake Chelsea!!

Nahodha wa Chelsea, John Terry, amewalaumu sana Wachezaji wenzake kufuatia kipigo chao cha Jumamosi cha mabao 3-1 walichoangushiwa na Timu 'dhaifu' Wigan ambayo katika mechi zake mbili za nyuma ilibugizwa 5-0 na Manchester United na 4-0 na Arsenal.Kipigo hicho toka kwa Wigan na ushindi wa Man U wa bao 2-0 dhidi ya Stoke City kumewafanya Man U ambao ndio Mabingwa Watetezi, kushika hatamu LIGI KUU England.Chelsea, ambao hawajachukua Ubingwa kwa miaka mitatu sasa tangu wautwae kwa mara mbili mfululizo chini ya Meneja Jose Mourinho, inaelekea wamekerwa sana na kipigo hicho na kufikia hatua ya kumfanya Terry kudiriki kuanika mzozo wao wa ndani ya Klabu hadharani.Terry amekaririwa akilalama: "Ni kawaida kucheza vibaya lakini hata ukicheza vibaya unategemea Wachezaji wenzako kujituma na kupigana! Timu nzima haikufanya hivyo! Timu kubwa zote zimeshinda wikiendi hii na hili linavunja moyo! Tuna mechi Jumatano, itabidi tufanye vizuri! Na Jumapili ijayo tuna mechi ngumu na Liverpool na itabidi tujitutumue!"
RATIBA YA SOKA WIKI HII:UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Jumanne, Septemba 29
Arsenal v OlympiakosAZ
Alkmaar v Standard
LiegeBarcelona v Dynamo
KievDebrecen v Lyon
Fiorentina v Liverpool
Rangers v SevillaRubin
Kazan v Inter Milan
Unirea Urziceni v VfB Stuttgart
Jumatano, Septemba 30
AC Milan v FC ZurichApoel
Nicosia v Chelsea
Byern Munich v Juventus
Bordeaux v Maccabi Haifa
CSKA Moscow v Besiktas
FC Porto v Atletico
Madrid
Manchester United v WolfsburgReal
Madrid v Marseille
EUROPA LIGI:Alhamisi,
Oktoba 1
Kuna jumla ya mechi 24 ila zinazotajwa hapa ni zile za Timu za Uingereza tu]BATE v EvertonCeltic v Rapid Vienna
Fulham v Basle
LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi, Oktoba 3
Bolton v Tottenham
Burnley v Birmingham
Hull City v Wigan
Manchester United v Sunderland
Wolverhampton v Portsmouth
Jumapili, Oktoba 4
Arsenal v Blackburn
Chelsea v Liverpool
Everton v Stoke City
West Ham v Fulham
Jumatatu, Oktoba 5
Aston Villa v Man City

Tuesday, September 22, 2009

Nyoka Mwenye Mkono Mmoja Awashangaza Wanasayansi China

Nyota aliyezaliwa akiwa na mkono mmoja nchini China amewashangaza wanasayansi nchini China. Kwa habari kamili kuhusiana na nyoka huyu GONGA World News pembeni kushoto.

Thursday, September 17, 2009

Akiri Adebayor kwa FA ‘kumtimba’ van Persie!!!


kwa ‘shingo upande’ kosa la aliloshitakiwa na FA la kutaka kumuumiza Mchezaji wa Arsenal Robin van Persie kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi iliyopita Uwanjani City of Manchester ambayo Man City waliishinda Arsenal 4-2.Refa wa mechi hiyo Mark Clattenburg hakuona kosa hilo lakini amekiri kwa FA, baada ya kushuhudia marudio ya video, kuwa angemlima Adebayor Kadi Nyekundu kama angeliona.Adebayor alipewa mpaka jana Jumatano ajitetee lakini ameamua kutofanya hivyo na kukubali kosa na adhabu atakayopewa ambayo inategemewa kuwa ni kufungiwa mechi 3 ya kwanza ikiwa ile ya Jumapili Man City watakapocheza na Man U.Adhabu hiyo itajulikana leo kesi hiyo itakaposikilizwa.Adebayor anakabiliwa na kosa jingine nalo ni la kuonyesha mwenendo usiokubalika wakati akishangilia goli lake siku hiyo hiyo Man City walipocheza na Arsenal na kwenda kuwachokoza Mashabiki wa Arsenal.Uamuzi wa kosa hili utajulikana Septemba 30.

Wednesday, September 16, 2009

Amerie&lil wayne schedule videoshoot around his new bay


The life of a baby maker is hard work, so when Amerie and Lil Wayne linked to shoot her latest video it had to be done in Los Angeles so he could be close to baby mama no. 3, Lauren London. The 24-year-old actress and the rapper welcomed a son Saturday night at Los Angeles’ Cedar Sinai Hospital.
“[When] we were doing the video they were ‘we have to figure it out because nature might take its course,” she told The BoomBox. “We were like ‘lets go to where nature might take its course [Los Angeles] so we can get a pick up shot in case he gets the call.” The video, which was shot earlier this month, is for the single ‘Heard Em All,’ off her upcoming album.
“He’s awesome,” she said of working with Wayne. “He’s always really, really nice. The first time I met him we were doing this event together and we were sitting in the stands. Our handlers were transporting us in the building or something, I just remember thinking ‘he’s really down to earth. He’s really cool.’ I’ve liked him ever since he was in Cash Money, in like ‘97. He’s always had a lot of charisma.”
Amerie is gearing up for the release of her fourth album ‘Love & War,’ her first on Def Jam Records. “[I'm] very excited about [the new album],” she said. “I love my fans [and] I really hope they love this album. I feel like they will if they loved the first one and the second one.”
Shouts to TheBoomBox, and I wonder if they are shooting the video with Wayne’s verse as we last heard that Weezy was only making a cameo.

Tuesday, September 15, 2009

Teem ya Man City wasubiri litakalomkuta Adebayor!!! Shabiki amlalamikia van Persie Polisi!!

Manchester City wanasubiri kujua hatima ya Mchezaji wao Emmanuel Adebayor kufuatia matukio mawili yanayomhusu yeye yalyotokea kwenye mechi ya LIGI KUU Jumamosi iliyopita ambayo Man City waliifunga Arsenal bao 4-2 Uwanjani City of Manchester.Tukio la kwanza ni ushangiliaji wa Adebayor alipofunga bao la 3 na kwenda kushangilia mbele ya Washabiki wa Arsenal ambao walikasirika na kutaka kuvamia uwanja lakini wakadhibitiwa na Walinzi pamoja na Polisi.Katika tukio hilo Mlinzi mmoja alipigwa kichwani na kupoteza fahamu kwa dakika 5 na Polisi wa Manchester wamesema Adebayor ndie chanzo cha fujo hizo.Refa Mark Clattenburg alimpa Adebayor Kadi ya Njano kwa tukio hilo.Tukio la pili ni pale Adebayor alipomgusa usoni Robin van Persie kwa buti na ingawa Refa hakuchukua hatua yeyote kwa Adebayor, van Persie alidai Adebayor alikusudia kumuumiza.Adebayor mwenyewe amekana hilo na kusema alimwomba radhi van Persie ambae amepinga hakuombwa radhi.FA wanatakiwa kutoa uamuzi kabla ya leo [Jumanne] saa 2 usiku [saa za bongo] kama watachukua hatua zozote kwa Adebayor na baada ya hapo Klabu inapewa masaa 24 kuamua kukata rufaa ikiwa adhabu imetolewa.Wakati huo huo, ameibuka Shabiki mmoja aliewakilisha malalamiko yake kwa Polisi kuwa van Persie aliwatukana alipokwenda mbele ya Mashabiki wa Man City baada ya kuifungia Arsenal goli dakika ya 62.Polisi wamesema wanachunguza malalamiko hayo.

UEFA yafuta kifungo cha Eduardo, huru kucheza kesho UEFA CHAMPIONS LEAGUE!!!

Rufaa ya Arsenal waliyokata kwa UEFA kupinga kwa adhabu ya Mshambuliaji wao mwenye asili ya Brazil lakini ni raia wa Croatia, Eduardo, aliyopewa kwa kumhadaa Refa Manuel Gonzalez katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Celtic hapo Agosti 26, imekubaliwa na UEFA na sasa adhabu ya kufungiwa mechi mbili imefutwa.Eduardu sasa ni ruksa kucheza mechi ya kesho ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ugenini Ubelgiji wakati Arsenal watakapokwaana na Standard Liege Uwanja wa Maurice Dufrasne.
yuleNahodha wa Everton Phillip Neville nje muda mrefu!!
Nahodha wa Everton, Phillip Neville, ambae ni mdogo wake Nahodha wa Manchester United, Gary Neville, atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia goti walipogongana na Dickson Etuhu wa Fulham katika mechi ya LIGI KUU siku ya Jumapili Uwanjani Craven Cottage na Fulham kushinda 2-1.Meneja wa Everton David Moyes amethibitisha habari hizo na kusema Neville ataenda kwa Wataalam Jijini London kwa uchunguzi zaidi na hapo ndipo watajua kwa uhakika muda gani atakosekana.

Sunday, September 13, 2009

mdau!! karibuni katika kiwanja kipya


kiwanja kipya cha funguliwa kinakwenda kwa jina la www.tanzania20.blospot.com

van persie adai emmanuel alimtimba makusudi ili amumize...!!!


Van Persie adai Adebayor alimtimba makusudi amuumize!!!=Adebayor huenda akasulubiwa na F.A kwa ushangiliaji!!!!

Emmanuel Adebayor, aliefunga bao moja dhidi ya Timu yake ya zamani Arsenal katika mechi ya jana ambayo Manchester City iliipiga Arsenal 4-2, huenda akawa matatani na FA hasa baada ya kufunga goli hilo la 3 na kisha kukimbia nusu ya Uwanja na kwenda mbele ya Mashabiki wa Arsenal kushangilia kitendo ambacho Refa alimpa Kadi ya Njano.Mashabiki hao wa Arsenal walichukizwa sana na kitendo hicho na ilibidi Polisi na Walinzi wawatulize.Ndani ya uwanja, Mchezaji wa Arsenal, Robben van Persie amedai Adebayor alimkanyaga usoni makusudi ingawa Adebayor mwenyewe amekiri hilo lakini amesema ni bahati mbaya na alimwomba radhi van Persie.Kitendo hicho hakikuonekana na Refa lakini van Persie amepinga kuwa Adebayor alimwomba radhi na aliendelea kung’ang’ania alitimbwa kusudi.

Tottenham 1 Manchester United 3
Manchester United, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, jana wakiwa ugenini mjini London Uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham, timu ambayo ilikuwa haijafungwa hata mechi moja msimu huu wa Ligi, jana mbali ya kujikuta iko nyuma kwa bao 1-0 lilofungwa sekunde ya 51 tangu mechi ianze na Jermaine Defoe na baadae ikijikuta inacheza watu 10 baada ya Mchezaji wao Mkongwe Paul Scholes kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, ilitoa soma la hali ya juu ya jinsi ‘Soka Bora na Tamu” linavyochezwa.Baada ya Manchester United kufungwa bao hilo moja walitulia na kutandaza soka la hali ya juu na kusawazisha bao hilo kupitia Mkongwe Ryan Giggs aliefunga kwa frikiki murua ambayo sasa itawafanya Washabiki wake wamsahau mpigaji frikiki wao wa kawaida Cristiano Ronaldo.Mbrazil Chipukizi Anderson, alieonyesha ukomavu mkuu katika kiungo, aliipatia Man U bao la pili na la kwanza kwake kwenye Ligi Kuu tangu ajiunge Man U.Hadi mapumziko Tottenham 1 Man U.Kipindi cha pili ndipo, Paul Scholes, baada ya tayari kuwa na Kadi moja ya Njano, alipewa Kadi ya pili ya Njano baada ya kuonekana amemchezea Rafu Tom Huddlestone ingawa marudio ya video yalionyesha ni Mchezaji wa Spurs ndie aliecheza rafu. Hiyo ilikuwa dakika ya 59 na Scholes akapewa Kadi Nyekundu.Hata hivyo, dakika ya 79, Wayne Rooney alifunga bao zuri baada ya kuihadaa ngome na Kipa Cudicini wa Spurs.Tottenham: Cudicini, Corluka, King, Bassong, Assou-Ekotto, Lennon, Huddlestone, Palacios, Defoe, Crouch, Keane. Akiba: Gomes, Hutton, Bentley, Jenas, Pavlyuchenko, Naughton, Kranjcar.Man Utd: Foster, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, Scholes, Anderson, Giggs, Berbatov, Rooney. Akiba: Kuszczak, Owen, Carrick, Nani, Fabio Da Silva, Jonathan Evans, Valencia.

Saturday, September 12, 2009

Wenger akiri: “Ni muhimu kumsimamisha Adebayor!”

Arsene Wenger amekiri kuwa ili Timu yake Arsenal iambulie chochote kwenye mechi ya leo ya Ligi Kuu England watakapocheza City of Manchester City Stadium na wenyeji Manchester City ni muhimu kumkaba Emmanuel Adebayor alieihama Arsenal na kwenda Man City msimu huu kwa vile ndie anaeng’ara sana kwa sasa.Adebayor msimu huu, katika mechi 3 za Man City Ligi Kuu ambazo wameshinda zote, amefunga goli katika kila mechi.Wenger vilevile ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni Mchezaji pekee ambae kiwango chake kilipanda juu sana kwa muda mfupi ni Adebayor ambae alimnunua kutoka Monaco mwaka 2006.Wenger amesema: “Tulimchukua kutoka Monaco akiwa hana namba huko na alipokuja kwetu kiwango chake kilipanda sana! Tunafurahia yote aliyotufanyia Arsenal na nadhani Klabu zote mbili, Arsenal na Man City, zimeridhika! Sisi tumepata pesa nzuri na wao wamepata Straika bora!”Mbali ya Adebayor, Man City pia imemchukua msimu huu Mlinzi Kolo Toure kutoka Arsenal ambae pia anang’ara na Timu yake mpya akiiongoza ngome ambayo katika mechi zao 3 za Ligi Kuu hawajafungwa hata goli moja.
Katika mechi ya leo, Man City itawakosa nyota wao Robinho na Tevez ambao wote waliumia katika mechi moja wakati Nchi zao Brazil na Argentina zilipokutana kwenye mechi ya Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita huko Rosario City, Argentina na Brazil kushinda 3-1.
Arsenal watamkosa majeruhi Andriy Arshavin lakini Nahodha wao Cesc Fabregas na Tomas Rosicky wapo fiti na huenda wakacheza.
Mechi kama hii msimu uliokwisha, Man City walishinda bao 3-0.
Refa katika mechi ya leo ni Mark Clattenburg.


FIFA yaizuia Chelsea kuwarudisha hata Wachezaji wao waliowatoa kwa mkopo!!

FIFA imewaambia Chelsea hawaruhisiwi kuwarudisha Wachezaji wao waliowatoa kwa Klabu nyingine kwa mkopo wa msimu mzima kufuatia kifungo chao cha kutosajili Wachezaji kwa vipindi viwili vya usajili ikimaanisha hawawezi kusajili hadi mwaka 2011 adhabu ambayo wamepewa baada ya kumchukua Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa kinyume cha taratibu.Ingawa Chelsea wana nia ya kukata rufaa kupinga adhabu hiyo, Meneja wao Carlo Ancelotti alitaka kupunguza makali ya adhabu hiyo kwa kuwarudisha Wachezaji wao Klabuni waliowatoa kwa mkopo akiwemo Mchezaji wa Timu ya Vijana ya England wa chini ya miaka 21 Michael Mancienne kutoka Wolves, Scott Sinclair toka Wigan na Muargentina Franco di Santo kutoka Blackburn.FIFA imetoa ufafanuzi kuwa ni Di Santo pekee anaeweza kurudi Stamford Bridge kwa vile mkopo wake ni nusu msimu lakini Sinclair haruhusiwi kurudi kwa vile mkopo wake ni wa msimu mzima na kuhusu Mancienne, ingawa mkopo wake ni wa msimu mzima, FIFA itatoa uamuzi baadae kuhusu kipengele cha mkataba ambacho kinatamka anaweza kurudi Chelsea kwa dharura.Mpaka sasa Chelsea wanangoja kupokea kutoka FIFA adhabu yao rasmi ndani ya siku 10 zijazo na kisha wanatakiwa ndani ya siku 21 kukata rufaa.Chelsea wametaka kuwarudisha Wachezaji hao iliowatoa kwa mkopo ili wawe kava ya akina Didier Drogba, Michael Essien, John Obi Mikel na Salomon Kalou ambao itawakosa mwezi Januari 2010 kwani wote wanategemewa kuwakilisha Nchi zao kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola.Hata hivyo Januari 2010, Chelsea wanategemea majeruhi wao wa muda mrefu Paulo Ferreira na Joe Cole kurudi uwanjani baada ya kupona magoti waliyoumia.

Friday, September 11, 2009

ULE MCHANANGE WA LIGI KUU England: Mechi za Wikiendi hii na taarifa zake mbalimbali

Emmanuel Adebayor atakuwa kivutio kikubwa wakati Klabu yake ya zamani Arsenal itakapotua City of Manchester Stadium kucheza na Wenyeji Manchester City hapo kesho.Adebayor, akiwa na Man City msimu huu, amefunga bao katika mechi zote 3 za Ligi Kuu walizocheza na kushinda zote.Katika mechi hizo 3, ngome ya Man City haijaruhusu hata bao moja na inaongozwa na Mchezaji mwingine alietoka Arsenal, Kolo Toure.Tottenham ni Klabu nyingine ambayo haijapoteza mechi msimu huu baada ya kushinda mechi zao zote 4 ikiwa na ile waliyoipiga Liverpool bao 2-1 siku ya ufunguzi wa mechi za Ligi Kuu lakini kesho wana mtihani mkubwa pale watakapowakaribisha Mabingwa watetezi Manchester United Uwanjani White Hart Lane.Chelsea, ambao ndio vinara wa Ligi baada ya mechi 4 na kushinda zote, kesho wapo safarini hadi Uwanja wa Britannia kupambana na Stoke City.Liverpool, ambao tayari katika mechi 4 wamepoteza mbili, watakwaana na Wababe wa Manchester United na Everton, Timu iliyopanda Daraja Burnley uwanjani Anfield. Hata hivyo, Burnley, wakicheza ugenini, hawajashinda wala kutoka droo na hawajafunga hata goli moja katika mechi zao mbili walizocheza huko ugenini.Huko katikati ya England, mjini Birmingham, kutakuwa na kindumbwendumbwe cha Watoto wa mji mmoja kukutana na mechi hii, kwa sababu za usalama, itachezwa saa 6 mchana kwa saa za Uingereza na kuwakutanisha Birmingham City na Aston Villa Uwanjani St Andrews. Villa ndio wanaoonekana wenye nguvu baada ya kushinda mechi zote 4 zilizopita kati yao ukiwemo ushindi wa mabao 5-1 Uwanjani Villa Park mwaka jana.Fulham wanawakaribisha Everton uwanjani Craven Cottage siku ya Jumapili huku Klabu zote zikitaka ushindi hasa baada ya kutoanza vizuri Ligi msimu huu. Fulham wameshinda mechi moja tu walipowafunga Portsmouth siku ya ufunguzi na wenzao Everton walifungwa mechi zao zote 2 za kwanza na kushinda ya 3 walipoiua Wigan.Portsmouth hawana pointi hata moja hadi sasa baada ya mechi 4 na wawakaribisha Bolton ambao nao pia wanasuasua baada ya kupoteza mechi zao zote 3.Blackburn Rovers , mpaka sasa wamecheza mechi 3 na kutoka droo moja na kufungwa mbili, wanawakaribisha Wolves uwanjani Ewood Park. Wolves wameanza msimu huu kwa kuwafunga Wigan, kutoka droo na Hull City na kufungwa na West Ham na Man City.Sunderland, walioshinda mechi 2 na kufungwa 2, watakuwa nyumbani Stadium of Light kucheza na Hull City ambao wamecheza mechi 4 na kushinda moja, droo moja na kufungwa 2.Wigan watakuwa wenyeji wa West Ham kwao DW Stadium msimu uliokwisha ilikuwa ikiitwa KC Stadium.Wigan wameshacheza mechi 4, wameshinda moja na kufungwa 3 wakati West Ham wana mechi 3 na wameshinda moja, droo moja na kufungwa moja.

LIGI KUU ENGLAND:

Jumamosi, 12 Septemba 2009
[mechi zote saa 11 jioni saa za bongo isipokuwa ikitajwa]Blackburn v WolverhamptonLiverpool v BurnleyMan City v ArsenalPortsmouth v BoltonStoke v ChelseaSunderland v HullTottenham v Man Utd [saa 1 na nusu usiku]Wigan v West HamJumapili, 13 Septemba 2009Birmingham v Aston Villa [saa 8 mchana]Fulham v Everton [saa 12 na robo]

Mechi za Vilabu zarudi tena!!

Baada ya mikiki na hekaheka, furaha kwa baadhi na huzuni kwa wengine katika Nchi zao mbalimbli zilizokuwa zikiwania kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010, sasa tunarudi kwenye michuano ya Klabu kwenye LIGI KUU England, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.Ifuatayo ni Ratiba ya Wiki moja kuanzia Jumamosi hii hadi Jumapili, Septemba 20.
Ramos ni Kocha wa CSKA Moscow
Kocha wa zamani wa Tottenham na Real Madrid Juande Ramos ameteuliwa Meneja wa CSKA Moscow na kumbadili Mbrazil Zico.Ramos, baada ya kutimuliwa Tottenham Oktoba, 2008, alipata kazi Real Madrid ya mkataba wa miezi 6 ulioisha mwishoni mwa msimu uliokwisha.CSKA Moscow wako Kundi moja pamoja na Manchester United kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Thursday, September 10, 2009

0, Paraguay waingia Fainali!!!


Paraguay leo alfajiri wameungana na Brazil kutoka Nchi za Marekani ya Kusini kuingia Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwapa kipigo cha bao 1-0 Argentina kwenye mechi iliyochezwa Paraguay.
Jumamosi, Argentina wakiwa nyumbani Rosario City, walipigwa bao 3-1 na Mahasimu wao wakubwa Brazil.
Bao la Paraguay lilifungwa na Haedo dakika ya 28.
Kwa kipigo hiki cha pili mfululizo ambacho mbali ya kuhatarisha sana nafasi ya Argentina kucheza Fainali huku zikiwa zimebaki mechi 2 tu kwenye Kundi lao, hata kibarua cha Kocha Diego Maradona sasa kina walakini mkubwa

Wednesday, September 9, 2009

David Gill wa Man U kachaguliwa katka chama cha Klabu Ulaya [ECA]!

Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, David Gill, amechaguliwa kwenye Bodi ya Chama cha Klabu Ulaya, ECA, [European Club Association] pamoja na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwa kipindi cha miaka miwili.
ECA ina Bodi hiyo yenye Wawakilishi 15 na hupeleka Wajumbe wake kwenye Kamati za UEFA na kushirikiana na kutoa ushauri kuhusu masuala ya Soka huko Ulaya.
ECA inaundwa kutokana na Klabu 144 toka Nchi 53 za Ulaya na hupigania haki za Vilabu hivyo huko Ulaya.

KOMBE LA DUNIA: England na Serbia wanachungulia Fainali!!

England na Serbia watatinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wakishinda mechi zao za leo Jumatano Septemba 9 na Spain, Denmark na Slovakia pia wanaweza kujihakikishia kucheza Fainali ikiwa, kwanza, watashinda na kisha mechi nyingine katika Makundi yao yaangukia upande wao na kuwasaidia.
England na Serbia zinaweza kufanya idadi ya Timu zilizotinga Fainali kufikia 10 ikiwa England itawafunga Croatia nyumbani Wembley Stadium katika KUNDI la 6 na Serbia wakiwafunga Ufaransa mbele ya Mashabiki wa Serbia kwenye Uwanja wa Marakana mjini Belgrade.
Mpaka sasa Timu zilizo Fainali ni Wenyeji Afrika Kusini, Uholanzi, Brazil, Ghana, Japana, Korea Kaskazini, Korea Kaskazini na Australia.
Huko Ulaya Washindi 9 wa kila Kundi wataenda Fainali na Timu 8 Bora zitakazoshika nafasi ya pili zitafanyiwa dro ili kuwe na mechi 4 na washindi wa mechi hizo wataingia Fainali.
Mabingwa wa Ulaya Spain wataingia Fainali wakiwafunga Estonia na wakati huo huo Turkey iwafunge Bosnia. Lakini hata Spain wakitoka droo na Turkey akishinda, Spain atenda Fainali.
Denmark atatinga Fainali ikiwa tu ataifunga Albania huku Portugal waifunge Hungary na Malta wasifungwe na Sweden.
Na kwa Slovakia, itabidi kwanza waombe Slovenia na Poland watoke suluhu kisha wao waifunge Ireland nyumbani kwao Belfast ndipo wataingia Fainali.
Mutu aomba atoe pesa kwenye Mifuko ya Hisani badala ya kuilipa Chelsea Pauni Milioni 15!!!!
**ASEMA HANA UWEZO KULIPA FAINI HIYO ILIYOWEKWA NA FIFA!
Adrian Mutu ametoa pendekezo ni bora achangie kwenye Mifuko ya Hisani au kwenye Mifuko yoyote inayowasaidia watu badala ya kuilipa Chelsea fidia ya Pauni Milioni 15 kama ilivyoamuliwa na FIFA na kuungwa mkono na CAS [Mahakama ya Usuluhishi Michezoni].
Mshambuliaji huyo kutoka Rumania alieigharimu Chelsea Pauni Milioni 15 mwaka 2003 alifukuzwa Chelsea mwaka mmoja baadae baada ya kugundulika anatumia cocaine na kufungiwa miezi 7 kutocheza soka.
FIFA iliamua Mutu ailipe Chelsea Pauni Milioni 15 ikiwa ni fidia lakini Mutu alikata rufaa kupinga uamuzi huo kwa Korti ya Usuluhishi Michezoni [CAS= Court of Arbitration for Sport].
Uamuzi wa CAS ulitolewa Julai mwaka huu na Mutu amebakiza muda wa wiki moja tu kukata Rufaa kwa Mahakama Kuu ya Uswisi ambayo ndiyo pekee yenye haki ya kusikiliza na kuamua maamuzi yanayotolewa na CAS.
Hatua ya Mutu ipo kwenye barua aliyowaandikia Chelsea, Kamati ya Nidhamu ya FIFA na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Katika barua hiyo, Mutu ameandika: “Siwezi kulipa kiasi hicho. Si suala la kuamua bali la kuelewa na kufahamu misingi ya kutokuwa na uwezo. Napendekeza nitoe mchango mkubwa utakaoamuliwa ili kuwasaidia Vijana wenye matatizo ya madawa ya kulevya na pia kutoa kiwango hicho hicho kwa Mfuko wa Hisani watakauchagua Chelsea wa mjini London na Nchini kwangu Romania.”
Baada ya kutimuliwa Chelsea, Mutu alijiunga na Juventus Januari 2005 kama Mchezaji huru na hivyo Chelsea kutopata hata senti na msimu mmoja baadae akaenda Fiorentina ambako yuko mpaka leo.


Tuesday, September 8, 2009

Rafa ajaribu kuwaonya Mawinga wake Babel na Riera

Rafa
Ryan Babel alitoka hadharani hivi karibuni na kusema bora aende kucheza kwao Uholanzi Timu ya Ajax ili ajihakikishie kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Uholanzi ili acheze Fainali za Kombe la Dunia kwa sababu akiwa Liverpool hana namba ya kudumu na hilo limemfanya asichukuliwe Timu ya Uholanzi katika mechi za hivi karibuni.Babel hakutajwa kwenye Kikosi cha Uholanzi kilichochaguliwa kucheza mechi za Kombe la Dunia Jumatano iliyopita ila aliitwa baadae baada ya Mshambuliaji mmoja kuumia.Inaelekea kauli ya Babel imemtibua Kocha Rafa Benitez ambae alitoka na kudai kuwa Babel na Riera wote wanalilia kucheza na wote wanacheza pozisheni moja hivyo kuna ushindani mkubwa.Benitez anasema: “Ujumbe ni rahisi tu. Kiwanjani kila Mchezaji lazima adhihirishe ana uwezo. Babel anajua hawezi kuhama kwa sasa. Ni lazima afanye kazi turidhike. Ni Mchezaji mzuri na ana kipaji. Ni muhimu tuongee nae na tuone anapata maendeleo gani.”
katika mchanange balaa la Wafaransa lawakumba Man City kwa kumpora Chipukizi!!!
Klabu ya Ufaransa Rennes imethibitisha kuwa wameishitaki Manchester City kwa FIFA kwa kumpora Chipukizi Jeremy Helan mwanzoni mwa mwaka huu.Mwaka 2008, Kijana huyo Helan, miaka 17, alitakiwa na Manchester United lakini Rennes wakagoma kumtoa na ndipo Man City wakajikita na kumchukua ingawa Rennes walidai wana mkataba na Helan kuwa atasaini mkataba mwingine kama Mchezaji wa Kulipwa akifikisha miaka 17.Huko Ufaransa hairuhsiwi mtoto chini ya miaka 18 kusaini mkataba wa kuwa Mchezaji wa Kulipwa wakati England wanaruhusiwa wakifikisha miaka 17.Hivi juzi tu FIFA imeifungia Chelsea hadi 2011 kutosajili Mchezaji baada ya kupatikana na hatia ya kumpora Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa.Siku mbili baadae ikaibuka Klabu nyingine ya Ufaransa Le Havre na kudai Manchester United imewapora Kijana wao Pogba kwa kuwarubuni Wazazi wake na kuwapa fedha taslimu na nyumba.Hata hivyo, ingawa Le Havre imedai imepeleka mashtaka FIFA, FIFA imesema haijapokea chochote na wakati huo huo Manchester United imewataka Le Havre waache madai hayo au la watawashitaki.Ingawa Rennes imepeleka kesi FIFA na wao pia wamepelekwa Mahakamani na upande wa Chipukizi Helan wakivutana kuhusu nini kilisainiwa wakati Helan alipojiunga na Rennes.
katika nyanja za makipa mmoja wa makipa, Kipa Paddy Kenny afungiwa Miezi 9 kwa kutumia madawa!!!!
Kipa wa Sheffield United inayocheza Daraja la Championship, chini tu ya Ligi Kuu, Paddy Kenny, miaka 31, amefungiwa kutocheza soka kwa miezi 9 kuanzia Julai 22, 2009 kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa ‘Ephedrine’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa zinazokatazwa kwa Wanasoka kwani huongeza nguvu.Paddy Kenny aligundulika kutumia dawa hiyo ambayo kawaida hutumika kutibu kifua hasa afueni kwenye pumu katika mechi Sheffield United walipocheza na Preston kwenye mechi maalum za mtoano kutafuta Timu kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu.Paddy Kenny amekiri kutumia dawa hiyo lakini alijitetea kuwa alikuwa akiumwa kifua.Kamati ya Sheria ya FA, Chama cha Soka England, imesema imeridhika na utetezi wa Kenny Paddy kuwa hakutumia ‘Ephedrine’ kuongeza nguvu na ndio maana hawakumpa adhabu kali ya kifungo cha miaka miwili lakini ni wajibu wao kutoa adhabu ili iwe fundisho kwa Wachezaji wa Kulipwa kutotumia dawa bila ya maelekezo ya Madaktari wa Klabu zao.Klabu ya Sheffield United imelalamika kuwa Kamati hiyo kwa sababu imekubali Kipa huyo hakutumia dawa hiyo kuongeza nguvu walitegemea adhabu ndogo zaidi au onyo au msamaha.
MAN U WAIONYA LE HAVRE!
Manchester United imeionya Klabu ya Le Havre ya Ufaransa kuwa watachukua hatua za kisheria ikiwa Klabu hiyo haitaacha kutoa madai kwamba waliwapa pesa Wazazi wa Chipukizi Paul Pogba, miaka 16, ili kijana huyo asaini kwao.Rais wa Le Havre, Jean-Pierre Louvel, amedai kuwa Manchester United iliwapa Wazazi wa Pogba, Baba na Mama, Pauni 87,000 kila mmoja pamoja na nyumba ya kuishi mjini Manchester.Louvel aliendelea na madai yake kwa kusema kuwa wameshapeleka malalimiko yao FIFA.Wiki iliyopita, FIFA iliifungia Chelsea hadi mwaka 2011 kutosajili Mchezaji yeyote baada ya kupatikana na hatia ya kumchukua Mchezaji chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lenz ya Ufaransa kinyume cha taratibu.Manchester United imesema imefuata taratibu zote za UEFA na FIFA na kwamba uhamisho huo ikiwa pamoja na Mikataba yake, ilipitiwa na kupasishwa na FA, Chama cha Soka England, pamoja na uongozi wa Ligi Kuu England. Vilevile, Man U walisisitiza kuwa kufuatana na kanuni za Klabu yao pamoja na sheria za soka wao hawawezi kutoa fedha au kuwanunulia nyumba Wzazi wa Mchezaji.Hata hivyo, inasemekana Chama cha Soka cha Ufaransa, kufuatia shinikizo la Le Havre, bado hakijatoa Cheti cha Kimataifa cha Uhamisho na ndio maana FIFA hawajaubariki uhamisho huo

KOMBE LA DUNIA: NCHI ZA ULAYA

RATIBA: Jumatano, 9 Septemba 2009
Albania v Denmark
,Andorra v Kazakhstan,
Armenia v Belgium,
Belarus v Ukraine,
Bosnia-Herzegovina v Turkey,
Czech Republic v San Marino,
England v Croatia,
Faroe Islands v Lithuania,
Germany v Azerbaijan,
Hungary v Portugal,
Israel v Luxembourg,Italy v Bulgaria,
Latvia v Switzerland,
Liechtenstein v Finland,
Malta v Sweden,
Moldova v Greece,
Montenegro v Cyprus,
Northern Ireland v Slovakia,
Norway v FYR Macedonia,
Romania v Austria,
Scotland v Netherlands,
Serbia v France,
Slovenia v Poland,
Spain v Estonia,
Wales v Russia,

Monday, September 7, 2009

Slaven Bilić adai kwamba wamegundua udhaifu wa England!!!!


Bilic
Kocha wa Croatia, Slaven Bilic, ambayo Timu yake inakutana na England Jumatano Uwanjani Wembley kwenye mechi muhimu ya mtoano ya kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia, amedai kuwa wamegundua udhaifu wa Timu ya England na watatumia mwanya huo siku hiyo ya Jumatano.Mpaka sasa, England, walio chini ya Kocha toka Italia, Fabio Capello, wanaongoza Kundi lao kwa kushinda mechi 7 katika 7 walizocheza na wako mbele ya timu ya pili Croatia kwa pointi 4 na pia wana mechi moja mkononi.England wakiifunga Croatia hiyo Jumatano watatinga Fainali Afrika Kusini.Croatia, walio nafasi ya pili Kundi hili, wamewazidi Timu ya 3, Ukraine, pointi 3 lakini Ukraine wana mechi moja mkononi.Hivyo, ni muhimu sana Croatia kuifunga England ingawa itakuwa mechi ngumu kwao hasa kwa vile katika mechi ya kwanza kati ya timu hizo, England waliwaumbua Croatia kwa kuwapigia bao 4-1 nyumbani kwao mjni Zagreb.Hata hivyo, Croatia wanapata matumaini hasa wakikumbuka Novemba, 2007, Uwanjani Wembley, walipowafunga England 3-2 na kuwang’oa England kuingia Fainali za EURO 2008.Slaven Bilic, enzi za Uchezaji wake alichezea West Ham mwaka 1996 na 1997 kisha kwenda kucheza Everton mwaka 1997 hadi 2000, amesema: “England kwa sasa ni Timu tofauti. Wana uzuri wao lakini kuna kitu kimepungua kwao. Sasa wanaukosa ule “Uingereza” ambao uliifanya iwe ngumu kufungika zamani! Lakini, tunajua nini hasa wanakikosa na siwezi kuwaambia ni nini! Ni siri yetu!”

Sunday, September 6, 2009

ARGENTINA 1 BRAZIL 3 NI MCHANANGE KATI YA MATAIFA MAWILI TOKA AMERICA YA KUSINI


KOMBE LA DUNIA: Argentina 1 Brazil 3


Brazil wamewanyuka Mahasimu wao wakubwa Argentina 3-1 wakiwa nyumbani kwao Rosario City katika mechi muhimu ya Kombe la Dunia na kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 na kuwaacha Argentina wamesambaratika na kutojua hatima yao.Mabao ya Brazil yalifungwa na Luisao, dakika ya 29, Faabiano bao 2 dakika ya 34 na 69.Bao la Argentina lilifungwa dakika ya 67.Argentina: Andujar; Zanetti, Dominguez, Otamendi, Heinze; Maxi, Mascherano, Veron, Datolo; Messi, Tevez. Akiba: Carrizo, Papa, Gago, Milito, Schiavi, Coloccini, Aguero.Brazil: Julio Cesar; Maicon, Lucio, Luisao, Andre Santos;Silva, Felipe Melo; Elano, Kaka; Robinho, Luis Fabiano. Akiba: Victor, Dani Alves, Miranda, Lucas, Ramires, Julio Baptista,Adriano.Refa: Julian Oscar Ruiz Acosta (Colombia.

Saturday, September 5, 2009

KOMBE LA DUNIA: Nini kinaendelea Makundi ya Afrika?


MECHI ZA LEO: Jumamosi Septemba 5

Gabon v CameroonTogo v MoroccoMozambique v KenyaNigeriav TunisiaRwanda v EgyptAlgeria v ZambiaGhana v SudanBenin v MaliMalawi v GuineaIvory Coast v Burkina FasoGhana inaweza kuwa Nchi ya kwanza Afrika kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na kuungana na Wenyeji Afrika Kusini ingawa mbali ya ushindi kwenye yao na sudan vilevile wanahitaji matokeo ya mechi nyingine Kundini kwao yaelekee kwao.Cameroon na Egypt wanahitaji pointi zote 3 katika mechi zao ili kuweka hai matumaini yao huku.Nigeria na Tunisia wanapambana na mshindi ndie atashika uongozi kwenye Kundi B.Ivory Coast walio Kundi E wakishinda mechi yao na Burkina Faso watahitaji pointi 1 tu ili waingie Fainali.
RATIBA KOMBE LA DUNIAULAYA
Jumamosi, 5 Septemba 2009Armenia v Bosnia-Herzegovina,Austria v Faroe Islands,Azerbaijan v Finland,Bulgaria v Montenegro,Croatia v Belarus,Cyprus v Rep of Ireland,Denmark v Portugal,France v Romania,Georgia v Italy,Hungary v Sweden,Iceland v Norway,Israel v Latvia,Moldova v Luxembourg,Poland v Northern Ireland,Russia v Liechtenstein,Scotland v FYR Macedonia,Slovakia v Czech Republic,Spain v Belgium,Switzerland v Greece,Turkey v Estonia,Ukraine v Andorra,
RATIBA KOMBE LA DUNIA NCHI ZA MAREKAJumamosi, 5 Septemba 2009-09-05Colombia v EcuadorPeru v UruguayParaguay v BoliviaArgentina v BrazilChile v Venezuela NI YA KUSINI

KIVUMBI LEO: Argentina V Brazil!!!


Brazil wabeba maji ya kunywa kwenda nayo Argentina!!!Timu ya Taifa ya Brazil imefungasha hadi maji yao ya kunywa kwa safari ya kwenda Argentina kupambana na wenyeji wao Argentina katika mechi muhimu sana ya mtoano ya Kombe la Dunia itakayochezwa leo saa 6 na nusu usiku [bongo taimu] Rosario City, Argentina.Mechi hii ni muhimu sana kwa Argentina hasa kwa vile wako nafasi ya 4 na pointi 5 nyuma ya Brazil wanaoongoza Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini ambalo litatoa Timu 4 kuingia Fainali na ya 5 itachuana na Timu moja toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Nchi za Caribean.Nyuma ya Argentina kwa pointi 2, kwenye nafasi ya 5, yuko Ecuador.Brazil wakishinda mechi ya leo na mechi nyingine kwenye Kundi hili yakienda upande wa Brazil basi Brazil atafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.Pengine Brazil wamekumbuka kauli ya Diego Maradona, ambae sasa ndie Kocha wa Argentina, aliyoitoa kwenye TV za Argentina kwamba kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990 huko Italia, Argentina walinyunyiza dawa za usingizi kwenye chupa ya maji ya Brazil. Argentina walishinda mechi hiyo 1-0 na kuwatoa mashindanoni Brazil.AFA, Chama cha Soka cha Argentina, kilipinga kauli hiyo ya Maradona lakini mpaka leo Brazil wanaamini maneno ya Maradona.Hata hivyo, Rodrigo Paiva, Afisa Habari wa Brazil, amepinga Brazil wanaogopa kudhuriwa na alisema hiyo ni tahadhari ya kawaida tu wanayoifanya kila wanaposafiri nje.Uhasimu kati ya Nchi mbili hizi za Marekani ya Kusini ni wa siku nyingi sana na mkubwa sana kiasi ambacho wengi wanaamini chochote kinaweza kutokea.

Mameneja wa Klabu Kubwa Ulaya wakutana Uswisi na UEFA


Kikao cha 11 cha Makocha Mahiri huko Ulaya pamoja na UEFA kinaendelea huko Nyon, Switzerland katika Jumba la Soka ya Ulaya na Mkurugenzi Mtendaji wa UEFA, Andy Roxburgh, amesema Kikao hicho ni kuwapa sauti Makocha na pia kuzungumzia masuala yanayohusu Marefa, Sheria, Mashindano na nini kinatokea Uwanjani.Roxburg akaongeza: “Kikao hiki kinasaidia Makocha Vijana kujifunza kutoka kwa Makocha “Wazee” na wazoefu kama Sir Alex Ferguson. Sisi UEFA tumetoa jukwaa na Makocha wanatupa taarifa na vilevile wanajadiliana miongoni mwao.”Kuhusu masuala ya Marefa, yupo aliekuwa Refa Mahiri sana, Pierluigi Collina, anaetoa ufafanuzi kwa Makocha kuhusu masuala yote ya Marefa.Vilevile, Makocha hao walijulishwa rasmi uamuzi wa UEFA wa kufanya majaribio ya kutumia Marefa wawili wa ziada kwenye mechi yatakayofanyika msimu huu kwenye mashindano ya EUROPA LIGI kuanzia hatua ya Makundi. Marefa hao wawili watakuwa wakisimama karibu na Magoli, mmoja katika kila goli, ili kumpa ushauri Refa wa nini kinatendeka kwenye boksi.Makocha waliohudhuria ni [kwenye Mabano Klabu zao:Arsène Wenger (Arsenal FC), Sir Alex Ferguson (Manchester United FC), Manuel Pellegrini (Real Madrid CF), Jesualdo Ferreira (FC Porto), Claude Puel (Olympique Lyonnais), Ciro Ferrara (Juventus), Laurent Blanc (FC Girondins de Bordeaux), Didier Deschamps (Olympique de Marseille), Felix Magath (FC Schalke 04), Thomas Schaaf (Werder Bremen), Martin Jol (AFC Ajax), Valeri Gazzaev (FC Dynamo Kyiv), Walter Smith (Rangers FC), Dan Petrescu (AFC Unirea Urziceni), Abel Resino (Club Atlético de Madrid), Henk Ten Cate (Panathinaikos FC) and Bernard Challandes (FC Zürich).

Chelsea yapata matumaini kidogo toka CAS, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni!!!!

Huenda Chelsea wakaruhusiwa kusaini Wachezaji wapya wakati Dirisha la Uhamisho likifunguliwa tena Januari 2010 mbali ya kuwa kifungoni hadi 2011 kutosajili Mchezaji kwa kukiuka sheria za usajili walipomchukua Chipukizi Gael Kakuta toka FC Lenz.Matumaini hayo yamekuja baada ya ufafanuzi kutoka CAS [Mahakama ya Usuluhishi Michezoni] kwamba endapo Chelsea watachelewesha kukata rufaa kwao na kuutumia muda wote wa kuwasilisha rufaa ndani ya siku 21, Mahakama hiyo itabidi icheleweshe kusikilizwa kesi hiyo na pia kuchelewa kutolewa uamuzi.Kawaida wakati Timu inapokata rufaa kwa CAS adhabu yao husimamishwa hadi uamuzi utolewe.Katibu Mkuu wa CAS, Mathieu Reeb, ametoa ufafanuzi: “Inategemea lini Chelsea wanakata Rufaa. Wakikata Rufaa wiki hii au ijayo, basi sisi tutapanga kusikiliza kesi Novemba na Desemba uamuzi utatoka. Lakini wakichelewesha na kutumia karibu siku zote 21 za kukata rufaa baada ya kupewa adhabu na FIFA, na sisi tutachelewa kuisikiliza na pengine kuto uamuzi baada ya Januari, 2010 na hivyo Chelsea wanaweza kusajili Januari, 2010 kwani kawaida adhabu husimama hadi uamuzi wetu.”Klabu ya Uswisi FC Sion ilikumbwa na mkasa kama wa Chelsea pale ilipomsajili Kipa wa Misri Essam El Hadary aliekuwa akichezea Al-Ahly na ikafungiwa kusajili na FIFA mwezi Aprili mwaka huu hadi 2010 lakini ikakata rufaa CAS na msimu huu imeruhusiwa kusajili kwani uamuzi wa rufaa yao utatoka baadae mwaka huu.Kawaida jopo linalosikiliza Rufaa huko CAS huwa na Majaji wawili, mmoja atateuliwa na Chelsea na mmoja na FC Lenz, wakati Mwenyekiti wa Jopo ni toka CAS.Uamuzi wowote wa CAS unaweza tu kukatiwa rufaa kwenye Mahakama Kuu ya Uswisi tu na si pengine popote.

Thursday, September 3, 2009

Sammy Lee apewa onyo na FA!!!!

Sammy Lee
Meneja msaidizi wa Liverpool, Sammy Lee, amepewa onyo na FA baada ya kukiri kosa la utovu wa nidhamu alipomkashifu Mwamuzi wa Akiba, Stuart Attwell, katika mechi ya Ligi Kuu kati ya Tottenham na Liverpool ambayo Liverpool walifungwa 2-1 na Sammy Lee kukasirishwa na Refa Phil Dowd kutowapa penalti.Sammy Lee, katika mechi hiyo, alitolewa uwanjani na Refa Phil Dowd baada ya kufarakana na Mwamuzi huyo Stuart Attwell.Kamisheni iliyosikiliza kesi hiyo ya Sammy Lee haikumpa adhabu kali kwa kuwa rekodi yake ni nzuri.Vilevile, Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, nae pia anayo kesi kwenye Kamisheni hiyo akituhumiwa kumkashifu Refa mara baada ya mechi hiyo hiyo na Tottenham.


LILE DIRISHA LA UHAMISHO LAFUNGWA!!!
Dirisha la Uhamisho lilifungwa rasmi Jumanne, Septemba 1 saa 1 usiku, saa za bongo, na Klabu za Ligi Kuu England zilitumia jumla ya Pauni Milioni 450 kununua Wachezaji, wakati msimu uliokwisha kipindi kama hiki zilitumia Pauni Milioni 500, na Klabu iliyoongoza katika manunuzi hayo ni Manchester City iliyotumia Pauni Milioni 120 ikiwa ni asilimia 27 ya jumla ya manunuzi ya Wachezaji kwa kununua Wachezaji 9.Klabu za Aston Villa, Liverpool, Sunderland na Tottenham zilitumia Pauni Milioni 25 kila mmoja kununua Wachezaji.Dirisha litakuwa wazi tena Januari 1, 2010.

Chelsea yapata kifungo toka FIFA, hairuhusiwi kusajili Mchezaji mpya hadi 2011!!!!!

Chelsea imefungiwa na FIFA kutosaini Mchezaji yeyote kwa vipindi viwili vya usajili baada ya kupatikana na hatia ya kumrubuni na kumsaini Kijana wa Kifaransa, Gael Kakuta, mwaka 2007 aliekuwa Klabu ya FC Lenz ya Ufaransa, kinyume cha taratibu.Mchezaji huyo amepigwa faini ya Euro 780,000 pamoja na kutoruhusiwa kucheza kwa miezi minne na Chelsea pia imetakiwa kuilipa fidia FC Lenz ya Euro 130,000.Kifungo cha Chelsea kutosaini Mchezaji mpya kinamaanisha hawawezi kuchukua Mchezaji yeyote hadi 2011.Madirisha ya Usajili ya FIFA ni Majira ya Joto, kati ya Mei na Agosti, na la pili ni lile la Januari.Gael Kakuta, miaka 18, yumo kwenye listi ya Wachezaji wa Chelsea waliosajiliwa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo ilipelekwa juzi tu UEFA.

Wednesday, September 2, 2009

Ranieri ateuliwa Maneja Roma huko Italia!!!

Ranieri
Meneja wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri, miaka 57, ameteuliwa kuwa Bosi mpya wa AS Roma ambayo iko Serie A huko Italia kuchukua nafasi ya Luciano Spalletti aliejiuzulu Jumanne iliyopita.Spalletti alichukua hatamu hapo AS Roma mwaka 2005 na kuiwezesha kushinda Kombe la Italia na kushika nafasi ya pili Serie A mwaka 2007 na 2008 lakini msimu uliopita walimaliza nafasi ya 6 na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE na badala yake wako EUROPA LIGI.Msimu huu katika mechi 2 za Ligi, Roma imefungwa zote na hilo likamfanya Spalletti ang’atuke.Ranieri aliiongoza Chelsea kati ya mwaka 2000 na 2004 na hivi karibuni alikuwa Juventus lakini akatimuliwa mwezi Mei baada ya Timu hiyo kucheza mechi 7 mfululizo bila ushindi.

UEFA yamfungia Eduardo mechi 2!!
Mshambuliaji wa Arsenal Eduardo amefungiwa mechi 2 na UEFA kwa kujidondosha makusudi kwenye mechi na Celtic na hivyo kumhadaa Refa ili apate penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 kwenye mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.Eduardo atazikosa mechi za Arsenal dhidi ya Standard Liege na Olympiakos za Makundi UEFA CHAMPIONS LEAGUE.Arsenal wamepewa siku 3 kuikatia rufaa adhabu hiyo.
Wadhamini FA Cup kujitoa!!
FA, Chama cha Soka England, kimetangaza Mdhamini wa Kombe la FA, E.On, hataongeza mkataba ukiisha mwaka 2010.E.On walikuwa na mkataba na FA wa miaka minne uliokuwa na thamani ya zaidi ya Pauni Milioni 32.

Mchezaji akatwa mguu baada ya kupigwa Radi kwenye mechi!!

Mchezaji wa Klabu ya FC Nordsjaelland ya Denmark, Jonathan Richter, amelazimika kukatwa mguu hospitali wiki 6 baada ya kupigwa na Radi akiwa uwanjani akiichezea Timu yake iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na Hvidovre.Madaktari walisema mguu wake uliharibika vibaya na kulikuwa hamna njia ila kuukata ili kumwokoa.