Wednesday, September 9, 2009

KOMBE LA DUNIA: England na Serbia wanachungulia Fainali!!

England na Serbia watatinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wakishinda mechi zao za leo Jumatano Septemba 9 na Spain, Denmark na Slovakia pia wanaweza kujihakikishia kucheza Fainali ikiwa, kwanza, watashinda na kisha mechi nyingine katika Makundi yao yaangukia upande wao na kuwasaidia.
England na Serbia zinaweza kufanya idadi ya Timu zilizotinga Fainali kufikia 10 ikiwa England itawafunga Croatia nyumbani Wembley Stadium katika KUNDI la 6 na Serbia wakiwafunga Ufaransa mbele ya Mashabiki wa Serbia kwenye Uwanja wa Marakana mjini Belgrade.
Mpaka sasa Timu zilizo Fainali ni Wenyeji Afrika Kusini, Uholanzi, Brazil, Ghana, Japana, Korea Kaskazini, Korea Kaskazini na Australia.
Huko Ulaya Washindi 9 wa kila Kundi wataenda Fainali na Timu 8 Bora zitakazoshika nafasi ya pili zitafanyiwa dro ili kuwe na mechi 4 na washindi wa mechi hizo wataingia Fainali.
Mabingwa wa Ulaya Spain wataingia Fainali wakiwafunga Estonia na wakati huo huo Turkey iwafunge Bosnia. Lakini hata Spain wakitoka droo na Turkey akishinda, Spain atenda Fainali.
Denmark atatinga Fainali ikiwa tu ataifunga Albania huku Portugal waifunge Hungary na Malta wasifungwe na Sweden.
Na kwa Slovakia, itabidi kwanza waombe Slovenia na Poland watoke suluhu kisha wao waifunge Ireland nyumbani kwao Belfast ndipo wataingia Fainali.
Mutu aomba atoe pesa kwenye Mifuko ya Hisani badala ya kuilipa Chelsea Pauni Milioni 15!!!!
**ASEMA HANA UWEZO KULIPA FAINI HIYO ILIYOWEKWA NA FIFA!
Adrian Mutu ametoa pendekezo ni bora achangie kwenye Mifuko ya Hisani au kwenye Mifuko yoyote inayowasaidia watu badala ya kuilipa Chelsea fidia ya Pauni Milioni 15 kama ilivyoamuliwa na FIFA na kuungwa mkono na CAS [Mahakama ya Usuluhishi Michezoni].
Mshambuliaji huyo kutoka Rumania alieigharimu Chelsea Pauni Milioni 15 mwaka 2003 alifukuzwa Chelsea mwaka mmoja baadae baada ya kugundulika anatumia cocaine na kufungiwa miezi 7 kutocheza soka.
FIFA iliamua Mutu ailipe Chelsea Pauni Milioni 15 ikiwa ni fidia lakini Mutu alikata rufaa kupinga uamuzi huo kwa Korti ya Usuluhishi Michezoni [CAS= Court of Arbitration for Sport].
Uamuzi wa CAS ulitolewa Julai mwaka huu na Mutu amebakiza muda wa wiki moja tu kukata Rufaa kwa Mahakama Kuu ya Uswisi ambayo ndiyo pekee yenye haki ya kusikiliza na kuamua maamuzi yanayotolewa na CAS.
Hatua ya Mutu ipo kwenye barua aliyowaandikia Chelsea, Kamati ya Nidhamu ya FIFA na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Katika barua hiyo, Mutu ameandika: “Siwezi kulipa kiasi hicho. Si suala la kuamua bali la kuelewa na kufahamu misingi ya kutokuwa na uwezo. Napendekeza nitoe mchango mkubwa utakaoamuliwa ili kuwasaidia Vijana wenye matatizo ya madawa ya kulevya na pia kutoa kiwango hicho hicho kwa Mfuko wa Hisani watakauchagua Chelsea wa mjini London na Nchini kwangu Romania.”
Baada ya kutimuliwa Chelsea, Mutu alijiunga na Juventus Januari 2005 kama Mchezaji huru na hivyo Chelsea kutopata hata senti na msimu mmoja baadae akaenda Fiorentina ambako yuko mpaka leo.


No comments:

Post a Comment