Saturday, September 5, 2009

Mameneja wa Klabu Kubwa Ulaya wakutana Uswisi na UEFA


Kikao cha 11 cha Makocha Mahiri huko Ulaya pamoja na UEFA kinaendelea huko Nyon, Switzerland katika Jumba la Soka ya Ulaya na Mkurugenzi Mtendaji wa UEFA, Andy Roxburgh, amesema Kikao hicho ni kuwapa sauti Makocha na pia kuzungumzia masuala yanayohusu Marefa, Sheria, Mashindano na nini kinatokea Uwanjani.Roxburg akaongeza: “Kikao hiki kinasaidia Makocha Vijana kujifunza kutoka kwa Makocha “Wazee” na wazoefu kama Sir Alex Ferguson. Sisi UEFA tumetoa jukwaa na Makocha wanatupa taarifa na vilevile wanajadiliana miongoni mwao.”Kuhusu masuala ya Marefa, yupo aliekuwa Refa Mahiri sana, Pierluigi Collina, anaetoa ufafanuzi kwa Makocha kuhusu masuala yote ya Marefa.Vilevile, Makocha hao walijulishwa rasmi uamuzi wa UEFA wa kufanya majaribio ya kutumia Marefa wawili wa ziada kwenye mechi yatakayofanyika msimu huu kwenye mashindano ya EUROPA LIGI kuanzia hatua ya Makundi. Marefa hao wawili watakuwa wakisimama karibu na Magoli, mmoja katika kila goli, ili kumpa ushauri Refa wa nini kinatendeka kwenye boksi.Makocha waliohudhuria ni [kwenye Mabano Klabu zao:Arsène Wenger (Arsenal FC), Sir Alex Ferguson (Manchester United FC), Manuel Pellegrini (Real Madrid CF), Jesualdo Ferreira (FC Porto), Claude Puel (Olympique Lyonnais), Ciro Ferrara (Juventus), Laurent Blanc (FC Girondins de Bordeaux), Didier Deschamps (Olympique de Marseille), Felix Magath (FC Schalke 04), Thomas Schaaf (Werder Bremen), Martin Jol (AFC Ajax), Valeri Gazzaev (FC Dynamo Kyiv), Walter Smith (Rangers FC), Dan Petrescu (AFC Unirea Urziceni), Abel Resino (Club Atlético de Madrid), Henk Ten Cate (Panathinaikos FC) and Bernard Challandes (FC Zürich).

No comments:

Post a Comment