Tuesday, September 15, 2009

Teem ya Man City wasubiri litakalomkuta Adebayor!!! Shabiki amlalamikia van Persie Polisi!!

Manchester City wanasubiri kujua hatima ya Mchezaji wao Emmanuel Adebayor kufuatia matukio mawili yanayomhusu yeye yalyotokea kwenye mechi ya LIGI KUU Jumamosi iliyopita ambayo Man City waliifunga Arsenal bao 4-2 Uwanjani City of Manchester.Tukio la kwanza ni ushangiliaji wa Adebayor alipofunga bao la 3 na kwenda kushangilia mbele ya Washabiki wa Arsenal ambao walikasirika na kutaka kuvamia uwanja lakini wakadhibitiwa na Walinzi pamoja na Polisi.Katika tukio hilo Mlinzi mmoja alipigwa kichwani na kupoteza fahamu kwa dakika 5 na Polisi wa Manchester wamesema Adebayor ndie chanzo cha fujo hizo.Refa Mark Clattenburg alimpa Adebayor Kadi ya Njano kwa tukio hilo.Tukio la pili ni pale Adebayor alipomgusa usoni Robin van Persie kwa buti na ingawa Refa hakuchukua hatua yeyote kwa Adebayor, van Persie alidai Adebayor alikusudia kumuumiza.Adebayor mwenyewe amekana hilo na kusema alimwomba radhi van Persie ambae amepinga hakuombwa radhi.FA wanatakiwa kutoa uamuzi kabla ya leo [Jumanne] saa 2 usiku [saa za bongo] kama watachukua hatua zozote kwa Adebayor na baada ya hapo Klabu inapewa masaa 24 kuamua kukata rufaa ikiwa adhabu imetolewa.Wakati huo huo, ameibuka Shabiki mmoja aliewakilisha malalamiko yake kwa Polisi kuwa van Persie aliwatukana alipokwenda mbele ya Mashabiki wa Man City baada ya kuifungia Arsenal goli dakika ya 62.Polisi wamesema wanachunguza malalamiko hayo.

No comments:

Post a Comment