Sunday, September 13, 2009

Tottenham 1 Manchester United 3
Manchester United, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, jana wakiwa ugenini mjini London Uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham, timu ambayo ilikuwa haijafungwa hata mechi moja msimu huu wa Ligi, jana mbali ya kujikuta iko nyuma kwa bao 1-0 lilofungwa sekunde ya 51 tangu mechi ianze na Jermaine Defoe na baadae ikijikuta inacheza watu 10 baada ya Mchezaji wao Mkongwe Paul Scholes kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, ilitoa soma la hali ya juu ya jinsi ‘Soka Bora na Tamu” linavyochezwa.Baada ya Manchester United kufungwa bao hilo moja walitulia na kutandaza soka la hali ya juu na kusawazisha bao hilo kupitia Mkongwe Ryan Giggs aliefunga kwa frikiki murua ambayo sasa itawafanya Washabiki wake wamsahau mpigaji frikiki wao wa kawaida Cristiano Ronaldo.Mbrazil Chipukizi Anderson, alieonyesha ukomavu mkuu katika kiungo, aliipatia Man U bao la pili na la kwanza kwake kwenye Ligi Kuu tangu ajiunge Man U.Hadi mapumziko Tottenham 1 Man U.Kipindi cha pili ndipo, Paul Scholes, baada ya tayari kuwa na Kadi moja ya Njano, alipewa Kadi ya pili ya Njano baada ya kuonekana amemchezea Rafu Tom Huddlestone ingawa marudio ya video yalionyesha ni Mchezaji wa Spurs ndie aliecheza rafu. Hiyo ilikuwa dakika ya 59 na Scholes akapewa Kadi Nyekundu.Hata hivyo, dakika ya 79, Wayne Rooney alifunga bao zuri baada ya kuihadaa ngome na Kipa Cudicini wa Spurs.Tottenham: Cudicini, Corluka, King, Bassong, Assou-Ekotto, Lennon, Huddlestone, Palacios, Defoe, Crouch, Keane. Akiba: Gomes, Hutton, Bentley, Jenas, Pavlyuchenko, Naughton, Kranjcar.Man Utd: Foster, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, Scholes, Anderson, Giggs, Berbatov, Rooney. Akiba: Kuszczak, Owen, Carrick, Nani, Fabio Da Silva, Jonathan Evans, Valencia.

No comments:

Post a Comment