Tuesday, September 8, 2009

Rafa ajaribu kuwaonya Mawinga wake Babel na Riera

Rafa
Ryan Babel alitoka hadharani hivi karibuni na kusema bora aende kucheza kwao Uholanzi Timu ya Ajax ili ajihakikishie kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Uholanzi ili acheze Fainali za Kombe la Dunia kwa sababu akiwa Liverpool hana namba ya kudumu na hilo limemfanya asichukuliwe Timu ya Uholanzi katika mechi za hivi karibuni.Babel hakutajwa kwenye Kikosi cha Uholanzi kilichochaguliwa kucheza mechi za Kombe la Dunia Jumatano iliyopita ila aliitwa baadae baada ya Mshambuliaji mmoja kuumia.Inaelekea kauli ya Babel imemtibua Kocha Rafa Benitez ambae alitoka na kudai kuwa Babel na Riera wote wanalilia kucheza na wote wanacheza pozisheni moja hivyo kuna ushindani mkubwa.Benitez anasema: “Ujumbe ni rahisi tu. Kiwanjani kila Mchezaji lazima adhihirishe ana uwezo. Babel anajua hawezi kuhama kwa sasa. Ni lazima afanye kazi turidhike. Ni Mchezaji mzuri na ana kipaji. Ni muhimu tuongee nae na tuone anapata maendeleo gani.”
katika mchanange balaa la Wafaransa lawakumba Man City kwa kumpora Chipukizi!!!
Klabu ya Ufaransa Rennes imethibitisha kuwa wameishitaki Manchester City kwa FIFA kwa kumpora Chipukizi Jeremy Helan mwanzoni mwa mwaka huu.Mwaka 2008, Kijana huyo Helan, miaka 17, alitakiwa na Manchester United lakini Rennes wakagoma kumtoa na ndipo Man City wakajikita na kumchukua ingawa Rennes walidai wana mkataba na Helan kuwa atasaini mkataba mwingine kama Mchezaji wa Kulipwa akifikisha miaka 17.Huko Ufaransa hairuhsiwi mtoto chini ya miaka 18 kusaini mkataba wa kuwa Mchezaji wa Kulipwa wakati England wanaruhusiwa wakifikisha miaka 17.Hivi juzi tu FIFA imeifungia Chelsea hadi 2011 kutosajili Mchezaji baada ya kupatikana na hatia ya kumpora Chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lens ya Ufaransa.Siku mbili baadae ikaibuka Klabu nyingine ya Ufaransa Le Havre na kudai Manchester United imewapora Kijana wao Pogba kwa kuwarubuni Wazazi wake na kuwapa fedha taslimu na nyumba.Hata hivyo, ingawa Le Havre imedai imepeleka mashtaka FIFA, FIFA imesema haijapokea chochote na wakati huo huo Manchester United imewataka Le Havre waache madai hayo au la watawashitaki.Ingawa Rennes imepeleka kesi FIFA na wao pia wamepelekwa Mahakamani na upande wa Chipukizi Helan wakivutana kuhusu nini kilisainiwa wakati Helan alipojiunga na Rennes.
katika nyanja za makipa mmoja wa makipa, Kipa Paddy Kenny afungiwa Miezi 9 kwa kutumia madawa!!!!
Kipa wa Sheffield United inayocheza Daraja la Championship, chini tu ya Ligi Kuu, Paddy Kenny, miaka 31, amefungiwa kutocheza soka kwa miezi 9 kuanzia Julai 22, 2009 kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa ‘Ephedrine’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa zinazokatazwa kwa Wanasoka kwani huongeza nguvu.Paddy Kenny aligundulika kutumia dawa hiyo ambayo kawaida hutumika kutibu kifua hasa afueni kwenye pumu katika mechi Sheffield United walipocheza na Preston kwenye mechi maalum za mtoano kutafuta Timu kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu.Paddy Kenny amekiri kutumia dawa hiyo lakini alijitetea kuwa alikuwa akiumwa kifua.Kamati ya Sheria ya FA, Chama cha Soka England, imesema imeridhika na utetezi wa Kenny Paddy kuwa hakutumia ‘Ephedrine’ kuongeza nguvu na ndio maana hawakumpa adhabu kali ya kifungo cha miaka miwili lakini ni wajibu wao kutoa adhabu ili iwe fundisho kwa Wachezaji wa Kulipwa kutotumia dawa bila ya maelekezo ya Madaktari wa Klabu zao.Klabu ya Sheffield United imelalamika kuwa Kamati hiyo kwa sababu imekubali Kipa huyo hakutumia dawa hiyo kuongeza nguvu walitegemea adhabu ndogo zaidi au onyo au msamaha.
MAN U WAIONYA LE HAVRE!
Manchester United imeionya Klabu ya Le Havre ya Ufaransa kuwa watachukua hatua za kisheria ikiwa Klabu hiyo haitaacha kutoa madai kwamba waliwapa pesa Wazazi wa Chipukizi Paul Pogba, miaka 16, ili kijana huyo asaini kwao.Rais wa Le Havre, Jean-Pierre Louvel, amedai kuwa Manchester United iliwapa Wazazi wa Pogba, Baba na Mama, Pauni 87,000 kila mmoja pamoja na nyumba ya kuishi mjini Manchester.Louvel aliendelea na madai yake kwa kusema kuwa wameshapeleka malalimiko yao FIFA.Wiki iliyopita, FIFA iliifungia Chelsea hadi mwaka 2011 kutosajili Mchezaji yeyote baada ya kupatikana na hatia ya kumchukua Mchezaji chipukizi Gael Kakuta kutoka FC Lenz ya Ufaransa kinyume cha taratibu.Manchester United imesema imefuata taratibu zote za UEFA na FIFA na kwamba uhamisho huo ikiwa pamoja na Mikataba yake, ilipitiwa na kupasishwa na FA, Chama cha Soka England, pamoja na uongozi wa Ligi Kuu England. Vilevile, Man U walisisitiza kuwa kufuatana na kanuni za Klabu yao pamoja na sheria za soka wao hawawezi kutoa fedha au kuwanunulia nyumba Wzazi wa Mchezaji.Hata hivyo, inasemekana Chama cha Soka cha Ufaransa, kufuatia shinikizo la Le Havre, bado hakijatoa Cheti cha Kimataifa cha Uhamisho na ndio maana FIFA hawajaubariki uhamisho huo

No comments:

Post a Comment