Saturday, October 31, 2009

NILIVYO ONA NILISHTUKA NIKA SEMA SIWEZI KUSITAJABU MIMI KUNA WADAUS






Mwanamke Ameza Uma na Vijiko 78Seti ya vijiko na uma vilivyotolewa toka kwenye tumbo lake

Uma ukitolewa toka kwenye tumbo lake wakati wa operesheni pembeni kulia ni baadhi ya vijiko na uma vilitolewa toka kwenye tumbo lake.

Madaktari nchini Ujerumani ilibidi wamfanyie operesheni ya dharura mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Margaret Daalman ambaye alikuwa akimeza vijiko na uma kila alipokuwa akila kwa muda mrefu kiasi cha kwamba jumla ya vijiko na uma 78 vilitolewa toka kwenye tumbo lake. Pichani Lundo la vijiko na uma vikiwa vimekusanyika kwenye tumbo lake. GONGA LIFE STYLE kwa habari zaidi.

Arsenal wawatoa nishai jirani zao Tottenham!!Arsenal 3 Tottenham 0

Katika dabi ya Timu za Kaskazini ya London, Arsenal wakiwa kwao Emirates Stadium waliwapiga Tottenham mabao 3-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema kuliko mechi nyingine za leo Jumamosi Oktoba 31.Mpaka mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa bao 2-0 kwa mabao yaliyofungwa ndani ya dakika moja katika dakika ya 43 Mfungaji akiwa Van Persie na la pili sekunde chache baadae kwa bao zuri sana la Nahodha Fabregas. Bao la 3 alifunga Van Persie.Vikosi:Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Fabregas, Song Billong, Diaby, Bendtner, van Persie, Arshavin. AKIBA: Mannone, Senderos, Nasri, Eduardo, Ramsey, Eboue, Gibbs. Tottenham: Gomes, Corluka, King, Bassong, Assou-Ekotto, Bentley, Huddlestone, Palacios, Jenas, Keane, Crouch. AKIBA: Button, Hutton, Bale, Pavlyuchenko, Dawson, Kranjcar, Woodgate. Refa: Mark Clattenburg .

Monday, October 26, 2009

Milan certain of Beckham deal


David Bekham.
AC Milan vice-president Adriano Galliani is "100% certain" David Beckham will return to the San Siro outfit in the winter transfer market.
The England midfielder has been strongly linked with a second loan spell at the Rossoneri to improve his chances of making Fabio Capello's FIFA World Cup™ squad.
Galliani told the Italian media: "Beckham's arrival is certain to happen, 100%. The agreement is done and all that is missing are the signatures."
The 34-year-old Beckham returned to the Los Angeles Galaxy in the summer after a successful six-month loan spell with Milan, where he helped the Rossoneri finish fourth in Serie A with two story by
www.fifa.com

Lil Wayne – Run This Town [No Ceilings]


Holy shit, this is some sick Lil Wayne right here! Weezy goes in over Jay-Z’s “Run This Town” beat and absolutely murders it! This track is also from the No Ceilings mixtape which is dropping in 6 .

Wednesday, October 21, 2009

Fergie asusa Mkutano na Waandishi baada ya swali kuhusu Refa Wiley!!

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson aligoma kuendelea na mkutano wa Waandishi wa Habari uliokuwa ukifanyika Uwanjani Luzhniki huko Moscow, Urusi baada ya kuulizwa swali kuhusu kesi yake na FA iliyotokana na kauli yake kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti.Ferguson amepewa na FA mpaka Novemba 3 kuwasilisha utetezi wake kuhusu mashitaka yanayohusiana na kesi hiyo.Baada ya kuulizwa swali kuhusu Refa Alan Wiley, Ferguson aliinuka na kutoka chumba cha mahojiano baada ya kutamka: “Swali la kipumbavu na halipati jibu! Nipo kwenye mkutano huu kuhusu mechi na CSKA Moscow!”
NI USIKU WA MAAJABU ULIKUWA JANA BARANI ULAYA!!!
MASKINI: Liverpool ni vipigo mfululizo!!!! Barca waaibishwa Nou Camp!!!
echi za jana za UEFA CHAMPIONS LEAGUE zimeleta matokeo yasiyotarajiwa na magoli bwelele huku ajabu kubwa ni pale Warusi Rubin Kazan walipowakung’uta Mabingwa Watetezi wa Ulaya FC Barcelona kwa bao 2-1 tena wakiwa nyumbani kwao Nou Camp.

Liverpool wameendelea kupata vipigo mfululizo ingawa jana sio puto ndio liliwafunga bali ni goli la dakika za majeruhi wakiwa kwenye ngome yao Anfield na pia kupata athari kubwa pale mhimili wao na Nahodha wao Steven Gerrard kucheza dakika 25 tu za mwanzo na kulazimika kutoka baada ya kuumia.
Matokeo ya mechi ya jana ambayo Liverpool alifungwa 2-1 na Lyon ya Ufaransa yamedhihirisha ile imani ya wengi kuwa Liverpool bila Gerrard na Torres ni nyanya tu. Jana Torres hakucheza kabisa.
Sasa, baada ya vipigo mfululizo, Jumapili kwenye Ligi Kuuu, Liverpool wanawakaribisha Mahasimu wao wakubwa Manchester United na hilo linawatia homa Mashabiki wa Liverpool.
Arsenal wakiwa ugenini huko Uholanzi na huku wakiongoza bao 1-0 walilazimishwa sare ya 1-1 na AZ Alkmaar.
Rangers ya Scotland iliadhiriwa vibaya ikiwa nyumbani baada ya kuchapwa bao 4-1 na Unirea Urziceni.
Sevilla, baada ya mechi 3 tu, wameweka rekodi huko Ulaya baada ya kufuzu kusonga mbele Raundi nyingine baada ya mechi 3 tu.
Matokeo kamili mechi za jana Jumanne, Oktoba 20:
KUNDI E
Liverpool 1 Lyon 2
Debrecen 3 Fiorentina 4
KUNDI F
Inter Milan 2 Dynamo Kiev 2
Barcelona 1 Rubin Kazan 2
KUNDI G
Stuttgart 1 Sevilla 3
Rangers 1 Unirea Urziceni 4
KUNDI H
AZ Alkmaar 1 Arsenal 1
Olympiakos 2 Standard Liege 1

Monday, October 12, 2009

Big Brother Revolution: Images from Day 35 - SUNDAY OCTOBER 11


Day 35 on M-Net’s Big Brother was all action on the Sunday show with the evictions of Hannington and Yacob PLUS the exit of SuperSport celebrity guest Thomas Mlambo AND a performance by Kenya’s award-winning star Amani. Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 for more entertainment 24/7 live. For more information log on to Pictured here are Elizabeth and Kevin.

Sunday, October 11, 2009

Wenger alicho ambiwa unakijua? "Wenger muda wa kusubiri umekwisha, leta Kombe Emirates"!!!


Arsene Wenger amejulishwa na Wamiliki wa Arsenal kuwa wamechoka kusubiri na msimu huu hamna subira na wanataka kuona Kombe linatua Uwanjani Emirates.Tangu wachukue Kombe la FA mwaka 2005, Arsenal hawajanyakua tena Kombe lolote lile ingawa kosakosa ni nyingi na wana Kikosi cha Vijana wanaotandaza ‘Soka Tamu’ linalovutia Ulaya nzima.Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema: “Ni lengo letu kuchukua Kikombe msimu huu! Kumaliza nafasi ya pili, tatu au nne si bora kwetu! Tuna imani tuna Kikosi kizuri!”Gazidis, mwenye asili ya Afrika Kusini, aliingizwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Arsenal Novemba 2008, amesisitiza kuwa ingawa Soka ni biashara kubwa haiweze kusahaulika kuwa Arsenal wapo hapo kwa ajili ya Mashabiki wao ambao hawajali Mahesabu mazuri ya Fedha bali hutaka ushindi uwanjani

Saturday, October 10, 2009

Ronaldo na Rooney Wataniana!!


Fowadi wa England, Wayne Rooney, ambae Timu yake ishafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani huku wakiwa wamebakisha mechi mbili amesema atafurahi sana ikiwa Cristiano Ronaldo na Ureno yake watashindwa kwenda Fainali hizo.Ureno iko hatarini kuzikosa Fainali hizo na wako nafasi ya 3 Kundini mwao pointi 2 nyuma ya Sweden walio nafasi ya pili huku Denmark akiongoza Kundi hilo.Rooney alisema: “Katika Kombe la Dunia mwaka 2006 Ureno walitung’oa Robo Fainali na mie nilipewa Kadi Nyekundu! Na tulipotolewa EURO 2008 Ronaldo alitucheka sana tulipokuwa nae Manchester United! Sasa bora wao wasiende Afrika Kusini!”Ronaldo alipoulizwa kuhusu kauli
ya Rooney alijibu kuwa anadhani rafiki yake huyo anawatania tu.

Fergie amwomba msamaha Refa Wiley

Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameomba msamaha kwa Refa Alan Wiley kwa kauli yake kwamba Refa huyo hayuko ‘fiti’ kuchezesha mechi kauli aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Manchester United na Sunderland iliyoisha 2-2 huko Old Trafford wikiendi iliyokwisha.Mara baada ya kauli hiyo ya Sir Alex Ferguson, FA, Chama cha Soka England, kilimwandikia barua Ferguson kumtaka ajieleze. Taarifa iliyotoka kwenye tovuti ya Manchester United imemkariri Ferguson akisema: “Naomba msamaha kwa Bw. Wiley kwa kumfedhehesha na kwa FA kwa kutoa mawazo yangu hadharani. Haikuwa nia yangu kumfanya Bw. Wiley amulikwe na Waandishi wa Habari. Nia yangu ni kukutana nae na kumwomba msamaha uso kwa uso mara nitakaporudi safari yangu nje ya Nchi.”Ferguson aliongeza kwamba anamheshimu Refa Wiley na kauli yake haikumaanisha:-Wiley ni Refa mbaya.-Wiley anapendelea.-Uamuzi wake kwenye mechi ile ulikuwa dhaifu.-Kwamba alipitwa na matukio muhimu kwenye mechi ile.Mara baada ya Ferguson kusema maneno kwamba Wiley ‘hayuko fiti’ mjadala na mzozo mkubwa uliibuka kwenye Vyombo vya Habari huko England
Daa!! Rio asema akiachwa Fainali Kombe la Dunia akiwa sio fiti halalamiki!!
Rio Ferdinand amesema akiikosa Fainali ya Kombe la Dunia mwakani kwa sababu hayuko fiti au ni majeruhi hawezi kulalamika kwa sababu Meneja wa sasa hajali majina bali huchagua Wachezaji fiti tu na walio kwenye fomu tu.Rio amezungumzia hilo hasa kwa vile yeye kwa sasa anasakamwa na majeruhi mfululizo yaliyomfanya katika mwaka huu acheze mechi 26 kati ya 40 angezoweza kuchezea Klabu yake Manchester United na England.Rio, atakaetimiza miaka 30 mwezi ujao, amesema: “Capello ni mkweli! Ameweka bayana anachagua mtu akiwa fiti na kwenye fomu tu na sio jina! Maishani sijaandamwa na majeruhi kama sasa! Na si tatizo moja tu linalonisumbua! Msimu uliokwisha niliumia mgongo, msimu huu nimeumia musuli nyuma ya ugoko na kisha musuli pajani! Ni vitu tofauti na sasa nafanyiwa mazoezi ili kujifua nisipate matatizo ya aina hii!”Rio Ferdinand anategemewa kucheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia ugenini na Ukraine.

Thursday, October 8, 2009

WADAU BONGO STAR SEARCH WATANGAZA ZAWADI!!!


Mkurugenzi wa Benchmark Production Rita Paulson(katikati)akiongea na waandishi wa habari juu ya kutangaza zawadi kwa washindi wa Bongo Star search(BSS)(kushoto)Brand Manager wa Kilimanjaro George Kavishe(kulia)Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania Emillian Rwejuna.Mashindano haya yatafanyika Diamond Jubilee Jumanne ijayo.

HABARI ZAIDI INGIA HAPA- http://www.fullshangwe.blogspot.com/
EBANAWEEE LISTI YA MAMENEJA MATAJIRI ENGLAND YATAJWA...?
Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Timu inayosuasua mkiani Daraja la Coca Cola Championship, Ipswich Town, anashikilia nafasi ya pili katika Listi ya Mameneja Matajiri huko England.Roy Keane amethaminiwa kuwa na utajiri wa Pauni Milioni 27.Anaeshika nambari wani ni Fabio Capello mwenye Pauni Milioni 30.Sir Alex Ferguson wa Manchester United ni wa tatu akiwa na Pauni Milioni 22.Listi ya Mameneja Matajiri 10 ni:
-Fabio Capello [England] Pauni Milioni 30-Roy Keane [Ipswich] Pauni Milioni 27-Sir Alex Ferguson [Manchester United] Pauni Milioni 22-Carlo Ancelotti [Chelsea] 17-Sven-Goran Eriksson [Notts County]-Arsene Wenger [Arsenal] 15-Harry Redknapp [Tottenham] 10-Rafael Benitez [Liverpool] 9-Martin O’Nell [Aston Villa] 9-Mark Hughes [Man City] 8

FIFA yairuhusu Man U kumsajili Kinda Pogba!!!

Pogba
Manchester United imeruhusiwa na FIFA kumsajili Kijana mdogo wa miaka 16 Paul Pogba baada ya Klabu ya Ufaransa Le Havre awali kuweka pingamizi kuwa Man U imempora Mchezaji huyo.Mwezi Septemba Chelsea ilifungiwa na FIFA kwa kumrubuni na kumsaini kinyume cha sheria Gael Kakuta mwaka 2007 na hivyo kupewa adhabu ya kutosajili Mchezaji yeyote hadi 2011.Lakini Jaji aliyeteuliwa na FIFA kuipitia kesi ya Le Havre na Manchester United kuhusu Paul Pogba aliamua kuwa kwa sababu Pogba ni mdogo haiwezekani kisheria Le Havre wawe na mkataba na Pogba kuichezea Klabu hiyo ya Ufaransa kama Mchezaji wa Kulipwa.Uamuzi huo wa FIFA umewaruhusu Manchester United kumsajili Pogba kwenye Chuo chao cha Soka.Mwezi uliokwisha Manchester United iliwatishia kuwashitaki Le Havre kwa kuwachafulia jina lao kwa madai kuwa wamemwiba Pogba.

FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009

Ebana wa FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Brazil, UAE na Germany zajikita Robo Fainali!!
MATOKEO MECHI ZA JANA
Jumatano, Oktoba 7
:Brazil 3 v Uruguay 1
Venezuela 1 v UAE 2
Germany 3 v Nigeria 2
ROBO FAINALI:09/10/09:
South Korea v Ghana 09/10/09
: Italy v Hungary 10/10/09
: Brazil v Germany 10/10/09
: UAE v Costa Rica

Tuesday, October 6, 2009

msani wa Bongo afanya vitu vyake ndani ya Big Brother

Ana kwenda kwa jina la A.Y kutoka viwanja vya bongo


Mmiliki wa Liverpool George Gillett amlaumu Rafael Benítez kwa matokeo mabaya!!!

George Gillett
George Gillett, mmoja wa Wamarekani wawili ambao ndio Wamiliki wa Liverpool amedai Rafael Benitez ndie alaumiwe kwa matokeo mabaya ya Liverpool ambao juzi walifungwa na Chelsea mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu. Gillett amedai yeye na Mmiliki mwenzake Tom Hicks wametoa dau la kutosha kuifanya Liverpool ipate Wachezaji bora na kuhakikisha mafanikio lakini kama hilo linaonekana haliwezekani basi wa kulaumiwa ni Benitez.Gillettte amesema: “Sisi tumewekeza pesa nyingi kupita hata Klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United!”
Refalii Mstaafu amponda Fergie!!!
FA wamtaka fergie kujieleza!!!
Jeff Winter ambae amestaafu baada ya kuwa mmoja wa Marefa wa Ligi Kuu England amemponda Sir Alex Ferguson kwa kauli yake aliyoitoa mara baada ya dro ya 2-2 ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland alipomsema Refa aliechezesha mechi hiyo Alan Wiley kuwa hayuko ‘fiti’.Jeff Winter amesema kauli za Ferguson ni za uburuzaji na kiwoga na pia amedai Ferguson alitoa kauli hizo ili kuficha ukweli kuwa Timu yake Man U ilicheza vibaya mechi hiyo. Winter amesema: “Nadhani safari hii Ferguson amezidisha na hili linaweza kuwaathiri Manchester United na huenda Marefa wakaungana na kuikomoa Timu hiyo kwenye mechi zao!” Klabu ya Manchester United imekataa kuzungumza lolote kuhusu kauli za Refa huyo wa zamani.Wakati huohuo, FA imemtaka Sir Alex Ferguson atoe ufafanuzi kuhusu kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fitiMmiliki wa Portsmouth auza hisa zake wiki 6 tu baada ya kuzinunua!!Sulaiman al-Fahim, ambae aliinunua Portsmouth wiki 6 zilizopita, ameamua kuuza aslimia 90 ya hisa hizo kwa Tajiri kutoka Saudi Arabia Ali al-Faraj.Uamuzi huo umekuja huku Klabu ya Portsmouth ikishindwa kuwalipa Wachezaji wake mishahara.Sulaiman al-Fahim ndie alishiriki kuinunua Klabu ya Manchester City kwa ajili ya Koo mojawapo ya Kifalme ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.

Saturday, October 3, 2009

VODACOM MISS TANZANIA 2009 NI MAGEUZI MAKUBWA,MREMBO KUTOKA MWANZA AJINYAKULIA TAJI TENA!!


Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald ambaye ni miss Mwanza pia akipungia mashabiki wake mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kartika shindano lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City na kushirikisha warembo wapatao 29 hivi baada ya mmoja wao kutolewa katika shindano hilo kutokana na kugundulika kuwa ni mjamzito.
Mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili umetoa mrembo wa Tanzania na kudhihirisha uwezo wake katika mashindano hayo makubwa na yenye mvuto nchini, Miriam anachukua nafasi ya Vodaciom Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim ambaye pia alitokea mkoani mwanza na kuufanya mkoa huo kuzichachafya kanada za Mkoa wa Dar es salaam Ilala Temeke na Kinondoni ambazo mara nyingi zimekuwa zikijitapa kuwa ndizo zenye warembo bomba kitu ambacho kimedhihirisha kuwa Tamb zao ni hazimzuii tembo kutoka Mwanza kunywa maji kisimani.
Miriam Gerald SALUYA44 anakutakia kila mafanikio katika kazi zako zote za Miss Tanzania ni kazi ngumu lakini ukiwa makini, ukajiheshimu na kusikiliza ushauri utashinda majaribu yoyote katika kazi hizo Mungu akujalie sana
Habari

Berbatov aliwahi kutekwa nyara?


Mshabuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, ametoboa kuwa miaka 10 iliyopita alitekwa nyara na Gangsta mkubwa huko kwao Bulgaria aitwae Georgi Iliev aliewatuma vibaraka wake watatu kumkamata ili kumlazimisha asaini Klabu ya Levski Kjustendil iliyomilikiwa na jambazi hilo.Wakati huo, Berbatov alikuwa Mchezaji wa CSKA Sofia huko Bulgaria.“Ni kweli!” Berbatov alithibitisha. “Ilitisha lakini nilifanikiwa kumpigia simu Baba yangu alieniokoa!”Akizungumzia presha anayoipata kwa kuchezea Klabu kubwa kama Manchester United, Berbatov alisema: “Ni presha kubwa! Sibishi kuwa mtu akilipa pesa nyingi kwa ajili yako anategemea vitu vikubwa toka kwako!”
Fergie na Torres ni Bora Septemba
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na Straika wa Liverpool, Fernando Torres, wameshinda Tuzo ya Ligi Kuu England ya Meneja Bora na Mchezaji Bora kwa mwezi Septemba.Sir Alex Ferguson ameshinda Tuzo ya Meneja Bora ikiwa ni mara yake ya 24 kuitwaa kwa kuiongoza Manchester United kushika uongozi kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda mechi zao zote za mwezi Septemba ambapo walianza kwa kuifunga Tottenham huko White Hart Lane 3-1, kisha kuwafunga Watani wao Man City 4-3 Old Trafford na kushinda Britannia Stadium 2-0 dhidi ya Stoke City.Man U vilevile walicheza mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwezi Septemba na kuifunga Besiktas 1-0 ugenini huko Ugiriki na pia kuilaza Wolfsburg Old Trafford 2-1.Fernando Torres ametunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora ikiwa ni mara yake ya pili kuipata kwa kufunga mabao matano mwezi Septemba. Torres, mpaka sasa, ndie anaeongoza kwa Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu akiwa na bao 8.