Wednesday, October 21, 2009

Fergie asusa Mkutano na Waandishi baada ya swali kuhusu Refa Wiley!!

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson aligoma kuendelea na mkutano wa Waandishi wa Habari uliokuwa ukifanyika Uwanjani Luzhniki huko Moscow, Urusi baada ya kuulizwa swali kuhusu kesi yake na FA iliyotokana na kauli yake kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti.Ferguson amepewa na FA mpaka Novemba 3 kuwasilisha utetezi wake kuhusu mashitaka yanayohusiana na kesi hiyo.Baada ya kuulizwa swali kuhusu Refa Alan Wiley, Ferguson aliinuka na kutoka chumba cha mahojiano baada ya kutamka: “Swali la kipumbavu na halipati jibu! Nipo kwenye mkutano huu kuhusu mechi na CSKA Moscow!”

No comments:

Post a Comment