Saturday, October 3, 2009

Berbatov aliwahi kutekwa nyara?


Mshabuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, ametoboa kuwa miaka 10 iliyopita alitekwa nyara na Gangsta mkubwa huko kwao Bulgaria aitwae Georgi Iliev aliewatuma vibaraka wake watatu kumkamata ili kumlazimisha asaini Klabu ya Levski Kjustendil iliyomilikiwa na jambazi hilo.Wakati huo, Berbatov alikuwa Mchezaji wa CSKA Sofia huko Bulgaria.“Ni kweli!” Berbatov alithibitisha. “Ilitisha lakini nilifanikiwa kumpigia simu Baba yangu alieniokoa!”Akizungumzia presha anayoipata kwa kuchezea Klabu kubwa kama Manchester United, Berbatov alisema: “Ni presha kubwa! Sibishi kuwa mtu akilipa pesa nyingi kwa ajili yako anategemea vitu vikubwa toka kwako!”

No comments:

Post a Comment