Tuesday, October 6, 2009

Refalii Mstaafu amponda Fergie!!!
FA wamtaka fergie kujieleza!!!
Jeff Winter ambae amestaafu baada ya kuwa mmoja wa Marefa wa Ligi Kuu England amemponda Sir Alex Ferguson kwa kauli yake aliyoitoa mara baada ya dro ya 2-2 ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland alipomsema Refa aliechezesha mechi hiyo Alan Wiley kuwa hayuko ‘fiti’.Jeff Winter amesema kauli za Ferguson ni za uburuzaji na kiwoga na pia amedai Ferguson alitoa kauli hizo ili kuficha ukweli kuwa Timu yake Man U ilicheza vibaya mechi hiyo. Winter amesema: “Nadhani safari hii Ferguson amezidisha na hili linaweza kuwaathiri Manchester United na huenda Marefa wakaungana na kuikomoa Timu hiyo kwenye mechi zao!” Klabu ya Manchester United imekataa kuzungumza lolote kuhusu kauli za Refa huyo wa zamani.Wakati huohuo, FA imemtaka Sir Alex Ferguson atoe ufafanuzi kuhusu kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fitiMmiliki wa Portsmouth auza hisa zake wiki 6 tu baada ya kuzinunua!!Sulaiman al-Fahim, ambae aliinunua Portsmouth wiki 6 zilizopita, ameamua kuuza aslimia 90 ya hisa hizo kwa Tajiri kutoka Saudi Arabia Ali al-Faraj.Uamuzi huo umekuja huku Klabu ya Portsmouth ikishindwa kuwalipa Wachezaji wake mishahara.Sulaiman al-Fahim ndie alishiriki kuinunua Klabu ya Manchester City kwa ajili ya Koo mojawapo ya Kifalme ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.

No comments:

Post a Comment