Saturday, October 3, 2009

Fergie na Torres ni Bora Septemba
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na Straika wa Liverpool, Fernando Torres, wameshinda Tuzo ya Ligi Kuu England ya Meneja Bora na Mchezaji Bora kwa mwezi Septemba.Sir Alex Ferguson ameshinda Tuzo ya Meneja Bora ikiwa ni mara yake ya 24 kuitwaa kwa kuiongoza Manchester United kushika uongozi kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda mechi zao zote za mwezi Septemba ambapo walianza kwa kuifunga Tottenham huko White Hart Lane 3-1, kisha kuwafunga Watani wao Man City 4-3 Old Trafford na kushinda Britannia Stadium 2-0 dhidi ya Stoke City.Man U vilevile walicheza mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwezi Septemba na kuifunga Besiktas 1-0 ugenini huko Ugiriki na pia kuilaza Wolfsburg Old Trafford 2-1.Fernando Torres ametunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora ikiwa ni mara yake ya pili kuipata kwa kufunga mabao matano mwezi Septemba. Torres, mpaka sasa, ndie anaeongoza kwa Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu akiwa na bao 8.

No comments:

Post a Comment