Saturday, October 3, 2009

VODACOM MISS TANZANIA 2009 NI MAGEUZI MAKUBWA,MREMBO KUTOKA MWANZA AJINYAKULIA TAJI TENA!!


Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald ambaye ni miss Mwanza pia akipungia mashabiki wake mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kartika shindano lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City na kushirikisha warembo wapatao 29 hivi baada ya mmoja wao kutolewa katika shindano hilo kutokana na kugundulika kuwa ni mjamzito.
Mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili umetoa mrembo wa Tanzania na kudhihirisha uwezo wake katika mashindano hayo makubwa na yenye mvuto nchini, Miriam anachukua nafasi ya Vodaciom Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim ambaye pia alitokea mkoani mwanza na kuufanya mkoa huo kuzichachafya kanada za Mkoa wa Dar es salaam Ilala Temeke na Kinondoni ambazo mara nyingi zimekuwa zikijitapa kuwa ndizo zenye warembo bomba kitu ambacho kimedhihirisha kuwa Tamb zao ni hazimzuii tembo kutoka Mwanza kunywa maji kisimani.
Miriam Gerald SALUYA44 anakutakia kila mafanikio katika kazi zako zote za Miss Tanzania ni kazi ngumu lakini ukiwa makini, ukajiheshimu na kusikiliza ushauri utashinda majaribu yoyote katika kazi hizo Mungu akujalie sana
Habari

No comments:

Post a Comment