Saturday, October 10, 2009

Ronaldo na Rooney Wataniana!!


Fowadi wa England, Wayne Rooney, ambae Timu yake ishafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani huku wakiwa wamebakisha mechi mbili amesema atafurahi sana ikiwa Cristiano Ronaldo na Ureno yake watashindwa kwenda Fainali hizo.Ureno iko hatarini kuzikosa Fainali hizo na wako nafasi ya 3 Kundini mwao pointi 2 nyuma ya Sweden walio nafasi ya pili huku Denmark akiongoza Kundi hilo.Rooney alisema: “Katika Kombe la Dunia mwaka 2006 Ureno walitung’oa Robo Fainali na mie nilipewa Kadi Nyekundu! Na tulipotolewa EURO 2008 Ronaldo alitucheka sana tulipokuwa nae Manchester United! Sasa bora wao wasiende Afrika Kusini!”Ronaldo alipoulizwa kuhusu kauli
ya Rooney alijibu kuwa anadhani rafiki yake huyo anawatania tu.

No comments:

Post a Comment