Saturday, October 10, 2009

Daa!! Rio asema akiachwa Fainali Kombe la Dunia akiwa sio fiti halalamiki!!
Rio Ferdinand amesema akiikosa Fainali ya Kombe la Dunia mwakani kwa sababu hayuko fiti au ni majeruhi hawezi kulalamika kwa sababu Meneja wa sasa hajali majina bali huchagua Wachezaji fiti tu na walio kwenye fomu tu.Rio amezungumzia hilo hasa kwa vile yeye kwa sasa anasakamwa na majeruhi mfululizo yaliyomfanya katika mwaka huu acheze mechi 26 kati ya 40 angezoweza kuchezea Klabu yake Manchester United na England.Rio, atakaetimiza miaka 30 mwezi ujao, amesema: “Capello ni mkweli! Ameweka bayana anachagua mtu akiwa fiti na kwenye fomu tu na sio jina! Maishani sijaandamwa na majeruhi kama sasa! Na si tatizo moja tu linalonisumbua! Msimu uliokwisha niliumia mgongo, msimu huu nimeumia musuli nyuma ya ugoko na kisha musuli pajani! Ni vitu tofauti na sasa nafanyiwa mazoezi ili kujifua nisipate matatizo ya aina hii!”Rio Ferdinand anategemewa kucheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia ugenini na Ukraine.

No comments:

Post a Comment