Thursday, October 8, 2009

FIFA yairuhusu Man U kumsajili Kinda Pogba!!!

Pogba
Manchester United imeruhusiwa na FIFA kumsajili Kijana mdogo wa miaka 16 Paul Pogba baada ya Klabu ya Ufaransa Le Havre awali kuweka pingamizi kuwa Man U imempora Mchezaji huyo.Mwezi Septemba Chelsea ilifungiwa na FIFA kwa kumrubuni na kumsaini kinyume cha sheria Gael Kakuta mwaka 2007 na hivyo kupewa adhabu ya kutosajili Mchezaji yeyote hadi 2011.Lakini Jaji aliyeteuliwa na FIFA kuipitia kesi ya Le Havre na Manchester United kuhusu Paul Pogba aliamua kuwa kwa sababu Pogba ni mdogo haiwezekani kisheria Le Havre wawe na mkataba na Pogba kuichezea Klabu hiyo ya Ufaransa kama Mchezaji wa Kulipwa.Uamuzi huo wa FIFA umewaruhusu Manchester United kumsajili Pogba kwenye Chuo chao cha Soka.Mwezi uliokwisha Manchester United iliwatishia kuwashitaki Le Havre kwa kuwachafulia jina lao kwa madai kuwa wamemwiba Pogba.

No comments:

Post a Comment