Tuesday, October 6, 2009

Mmiliki wa Liverpool George Gillett amlaumu Rafael Benítez kwa matokeo mabaya!!!

George Gillett
George Gillett, mmoja wa Wamarekani wawili ambao ndio Wamiliki wa Liverpool amedai Rafael Benitez ndie alaumiwe kwa matokeo mabaya ya Liverpool ambao juzi walifungwa na Chelsea mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu. Gillett amedai yeye na Mmiliki mwenzake Tom Hicks wametoa dau la kutosha kuifanya Liverpool ipate Wachezaji bora na kuhakikisha mafanikio lakini kama hilo linaonekana haliwezekani basi wa kulaumiwa ni Benitez.Gillettte amesema: “Sisi tumewekeza pesa nyingi kupita hata Klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United!”

No comments:

Post a Comment