Sunday, October 11, 2009

Wenger alicho ambiwa unakijua? "Wenger muda wa kusubiri umekwisha, leta Kombe Emirates"!!!


Arsene Wenger amejulishwa na Wamiliki wa Arsenal kuwa wamechoka kusubiri na msimu huu hamna subira na wanataka kuona Kombe linatua Uwanjani Emirates.Tangu wachukue Kombe la FA mwaka 2005, Arsenal hawajanyakua tena Kombe lolote lile ingawa kosakosa ni nyingi na wana Kikosi cha Vijana wanaotandaza ‘Soka Tamu’ linalovutia Ulaya nzima.Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema: “Ni lengo letu kuchukua Kikombe msimu huu! Kumaliza nafasi ya pili, tatu au nne si bora kwetu! Tuna imani tuna Kikosi kizuri!”Gazidis, mwenye asili ya Afrika Kusini, aliingizwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Arsenal Novemba 2008, amesisitiza kuwa ingawa Soka ni biashara kubwa haiweze kusahaulika kuwa Arsenal wapo hapo kwa ajili ya Mashabiki wao ambao hawajali Mahesabu mazuri ya Fedha bali hutaka ushindi uwanjani

No comments:

Post a Comment