
DA! TUPO PAMOJA WADAU KATIKA IDD ALL- KHAJI
PANAPO MAJALIWA YA MWENYEZI MUNGU KESHO SIKUKU NDUGU ZANGU WOTE WAISLAM SALUYA44 INAKUTAKIA IDD ALL-KHAJI NZURI KABISA NA WEEK END NJEMA.. SINA MENGI KWA WADAU WANGU.
Afrika kujua leo Nchi 3 zitakazoungana na Wenyeji Afrika Kusini, Ghana na Ivory Coast Fainali!!!
Yule Boss wa England, Fabio Capello, amesema Kikosi chake hakina nafasi kwa Mchezaji ambae hayuko fiti na wasitegemea watachukuliwa kwenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani ikiwa hawakuthibitisha uimara wao.Capello anategemewa kutangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil Jumamosi tarehe 14 Novemba 2009 huko Doha, Qatar muda wowote leo.Capello amemzungumzia Rio Ferdinand na kusema ikiwa atakuwa fiti kabla hajateua Kikosi chake cha mwisho basi ataenda nae Afrka Kusini lakini ameonya kuwa Ledley King, Beki wa Tottenham, na Kipa David James wana mashaka makubwa kutokana na kuwa majeruhi.Kuhusu David James, Capello alisema: "James anacheza vizuri lakini tangu aumie akicheza mechi baadae hawezi kufanya mazoezi siku mbili.


Daktari wa operesheni za urembo za kurekebisha maumbile wa nchini Ujerumani Reza Vossough, amejitamba jinsi alivyomuoa mwanamke asiye na mvuto wowote na kumfanyia operesheni kila kona ya mwili wake kumgeuza mwanamke mwenye mvuto kwa jinsi alivyotaka yeye. Pichani Cany Vossough alivyo sasa baada ya operesheni kibao za kurekebisha maumbile yake. Gonga Life Style Pembeni kushoto kusoma habari kamili.