Monday, August 31, 2009

LIGI KUU ENGLAND kusitishwa wiki 2 kupisha Mitoano KOMBE LA DUNIA!!!

Baada ya kuchezwa mechi za jana Jumapili, LIGI KUU itasimama kwa wiki mbili na kurudi tena tarehe 12 Septemba 2009 ili kupisha mechi za Timu za Taifa za kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.Mechi hizo za Mataifa zitachezwa tarehe 5 Septemba na tarehe 9 Septemba.RATIBA YA LIGI KUU ni kama ifuatavywo:JUMAMOSI, 12 Septemba 2009 [SAA ZA BONGO][saa 11 jioni]Blackburn v WolverhamptonLiverpool v BurnleyMan City v ArsenalPortsmouth v BoltonStoke v ChelseaSunderland v HullWigan v West ham[saa 1 na nusu usiku]Tottenham v Man UJUMAPILI, 13 Septemba 2009[saa 8 mchana]Birmingham v Aston Villa[saa 12 na robo]Fulham v Everton.KikoCapello ateua si cha England!! Kocha wa England Fabio Capello ametangaza Kikosi chake kitakachopambana na Slovenia kwa mechi ya kirafiki hapo Jumamosi na mechi ya mtoano wa Kombe la Dunia dhidi ya Croatia Jumatano Septemba 5.Peter Crouch, Aaron Lennon na Wes Brown wameitwa tena Kikosini baada ya kukosekana katika mechi za hivi karibuni za Timu hiyo.Lakini Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen hakuitwa pamoja na Maveterani wa Timu hiyo Kipa David James na Mlinzi Rio Ferdinand ambao ni majeruhi.England watacheza na Slovenia Wembley saa moja na nusu usiku, saa za bongo, hapo Jumamosi, na Jumatano, Septemba 5 mechi na Croatia itakuwa saa 4 usiku saa za bongo.Endapo England wataifunga Croatia hiyo Jumatano watajihakikishia kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.KIKOSI KAMILI:Makipa: Foster (Manchester United), Green (West Ham), Robinson (Blackburn)Walinzi: Johnson (Liverpool), Brown (Manchester United), Upson (West Ham), Terry (Chelsea), Lescott (Manchester City), A Cole (Chelsea), Bridge (Manchester City)Viungo: Wright-Phillips (Manchester City), Lennon (Tottenham), Beckham (Los Angeles Galaxy), Barry (Manchester City), Lampard (Chelsea), Carrick (Manchester United), Gerrard (Liverpool), A Young (Aston Villa), Milner (Aston Villa)Washambuliaji: Rooney (Manchester United), Heskey (Aston Villa), Defoe (Tottenham), C Cole (West Ham), Crouch (Tottenham

Friday, August 28, 2009

Villa nje, Fulham, Everton wapeta EUROPA LIGI!!!

Licha ya kufungwa ugenini bao 1-0 na Amkar Perm ya Urusi, Fulham imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI kwa jumla ya mabao 3-2 huku wenzao Everton wakijumuika nao baada ya pia kuwa ugenini na kutoka suluhu ya 1-1 na Sigma Olomouc ya Czech Republic na kutinga kwenye Makundi kwa jumla ya mabao 5-1.Kwa Aston Villa, licha ya kushinda uwanjani kwao 2-1 dhidi ya Rapid Vienna ya Austria, Villa imebwagwa nje ya EUROPA LIGI kwa bao la ugenini kwani ilifungwa mechi ya kwanza bao 1-0 na hivyo jumla ya mabao kuwa 2-2 katika mechi mbili.Droo ya kuamua Timu zipi zitakuwa Kundi lipi itafanywa leo huko Monaco kabla ya mechi ya leo kugombea SUPER CUP kati ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Barcelona, na Bingwa wa UEFA CUP, Shakhtar Donetsk.

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUEKlabu 5 za Uingereza zimewekwa kwenye Makundi ambayo Wadau wengi wamedai ni “laini kidogo” baada ya kuepuka kupangwa na Timu Vigogo wa Ulaya. Manchester United ambao walifika Fainali msimu uliopita wapo pamoja na CSKA Moscow, Besiktas na Wolfsburg KUNDI B.Liverpool watamenyana na Lyon, Fiorentina na Debrecen wakati Chelsea wapo na Porto, Atletico Madrid na APOEL Nicosia.Arsenal wamepangiwa na AZ Alkmaar, Olympiakos na Standard Liege wakati Rangers ya Scotland itacheza na Stuttgart, Sevilla na Unirea Urziceni.Klabu za England zimekwepa kuwekwa na Real Madrid na Inter Milan huku Real akiwa Kundi moja na AC Milan, Marseille na FC Zurich.Inter Milan yuko pamoja na Barcelona, Dynamo Kiev na Rubin Kazan.Msimu uliokwisha Chelsea walitolewa nje na Brcelona kwenye Nusu Fainali kwa bao la Andres Iniesta la dakika za majeruhi na Mkurugenzi Mtendaji wao Peter Kenyon alizungumza baada ya upangaji Makundi na kusema: “Tunaanza upya na siku zote tunataka twende mbele zaidi. Hamna mechi rahisi au Kundi laini lakini tumewakwepa Vigogo!!”Manchester United, kwa kuwa Kundi moja na CSKA Moscow, watarudi tena Uwanja wa Luzhniki walipowatoa Chelsea Fainali ya 2008 na kuwa Bingwa wa Ulaya na Mkuurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo David Gill ametamka: “Kwa ujumla, tunafurahia Kundi letu. Tuna shauku kubwa kurudi tena Moscow baada ya furaha ya 2008!”Lakini, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alisema: “CSKA sasa wamejijenga sana na mechi za kuchezea Uturuki ni ngumu siku zote. Pia tunajua ubora wa Wolfsburg na mafanikio yao Bundesliga msimu uliopita.”Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Liverpool, Christian Purslow, amesema: “Tumefurahia!”Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alionyesha tahadhari kuhusu KUNDI H ambalo wao wapo na kutamka: “Wengine wataangalia na kusema Arsenal atapita lakini tupo makini. Itakuwa ngumu ila tutatimiza kazi yetu.”Yapo Makundi Manane yenye Timu 4 kila moja na mechi zitachezwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 15 na 16.Washindi wanane wa kila Kundi pamoja na Washindi wa pili wataingia hatua ya mtoano huku washindi wa tatu wakiingizwa EUROPA LIGI.Fainali itachezwa Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium tarehe 22 May 2010 ambayo ni Jumamosi tofauti na hapo nyuma Fainali kuchezwa Jumatano.

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUEKlabu 5 za Uingereza zimewekwa kwenye Makundi ambayo Wadau wengi wamedai ni “laini kidogo” baada ya kuepuka kupangwa na Timu Vigogo wa Ulaya. Manchester United ambao walifika Fainali msimu uliopita wapo pamoja na CSKA Moscow, Besiktas na Wolfsburg KUNDI B.Liverpool watamenyana na Lyon, Fiorentina na Debrecen wakati Chelsea wapo na Porto, Atletico Madrid na APOEL Nicosia.Arsenal wamepangiwa na AZ Alkmaar, Olympiakos na Standard Liege wakati Rangers ya Scotland itacheza na Stuttgart, Sevilla na Unirea Urziceni.Klabu za England zimekwepa kuwekwa na Real Madrid na Inter Milan huku Real akiwa Kundi moja na AC Milan, Marseille na FC Zurich.Inter Milan yuko pamoja na Barcelona, Dynamo Kiev na Rubin Kazan.Msimu uliokwisha Chelsea walitolewa nje na Brcelona kwenye Nusu Fainali kwa bao la Andres Iniesta la dakika za majeruhi na Mkurugenzi Mtendaji wao Peter Kenyon alizungumza baada ya upangaji Makundi na kusema: “Tunaanza upya na siku zote tunataka twende mbele zaidi. Hamna mechi rahisi au Kundi laini lakini tumewakwepa Vigogo!!”Manchester United, kwa kuwa Kundi moja na CSKA Moscow, watarudi tena Uwanja wa Luzhniki walipowatoa Chelsea Fainali ya 2008 na kuwa Bingwa wa Ulaya na Mkuurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo David Gill ametamka: “Kwa ujumla, tunafurahia Kundi letu. Tuna shauku kubwa kurudi tena Moscow baada ya furaha ya 2008!”Lakini, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alisema: “CSKA sasa wamejijenga sana na mechi za kuchezea Uturuki ni ngumu siku zote. Pia tunajua ubora wa Wolfsburg na mafanikio yao Bundesliga msimu uliopita.”Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Liverpool, Christian Purslow, amesema: “Tumefurahia!”Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alionyesha tahadhari kuhusu KUNDI H ambalo wao wapo na kutamka: “Wengine wataangalia na kusema Arsenal atapita lakini tupo makini. Itakuwa ngumu ila tutatimiza kazi yetu.”Yapo Makundi Manane yenye Timu 4 kila moja na mechi zitachezwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 15 na 16.Washindi wanane wa kila Kundi pamoja na Washindi wa pili wataingia hatua ya mtoano huku washindi wa tatu wakiingizwa EUROPA LIGI.Fainali itachezwa Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium tarehe 22 May 2010 ambayo ni Jumamosi tofauti na hapo nyuma Fainali kuchezwa Jumatano.

UHAMISHO LIGI KUU ENGLAND!!!!!

Zikiwa zimebaki siku chache kabla dirisha la uhamisho halijafungwa hapo Agosti 31, spidi ya uhamisho imepamba moto huku Klabu nyingi bado zikichacharika kusaka Wachezaji.Baadhi ya biashara zilizokamilika hivi karibuni ni pamoja na uhamisho wa Mlinzi na Nahodha wa Manchester City Richard Dunne, miaka 29, kuhamia Aston Villa.Aston Villa pia imemchukua Stephen Warnock, miaka 27,kutoka Blackburn Rovers kwa mkataba wa miaka minne.Warnock, anaeweza kucheza kama Kiungo au Beki wa kushoto, alijiunga na Blackburn mwaka 2007 akitokea Liverpool.Mlinzi wa Portsmouth Sylvain Distin, miaka 31, amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitatu na ada ambayo haikutajwa.Nao Wachezaji wa Middlesbrough iliyoshushwa Daraja msimu uliokwisha, Robert Huth, mlinzi kutoka Ujerumani na Tuncay Sanli wa Uturuki, wamejiunga na Stoke City.Blackburn Rovers wamemsaini Pascal Chimbonda kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Tottenham Hotspur.

Bayern Munich wamchota Robben!

Real Madrid wamekubali kumuuza Winga wa zamani wa Chelsea, Mdachi Arjen Robben, kwa Bayern Munich kwa ada ya Pauni Milioni 22.Robben, miaka 25, alitegemewa kuhama Real tangu Klabu hiyo iwanunue Cristiano Ronaldo na Kaka.Nae Bosi mkubwa wa Bayern Munich, Hoeness, ametamka: “Robben ataimarisha Timu. Yeye akicheza Winga kulia na Ribery kushoto Timu itakuwa bomba!”

Wednesday, August 26, 2009

Wenger: “Leo na Celtic ni Mechi Kubwa kupita Jumamosi na Man U!!!”

Meneja wa Arsenal,Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametamka mechi ya leo ya marudiano ya mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Timu yake Arsenal na Celtic itakayochezwa nyumbani kwa Arsenal Emirates Stadium ni mechi kubwa kupita mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England watakayocheza Old Trafford na Mabingwa Manchester United.Arsenal waliishinda Celtic mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0 na suluhu ya aina yeyote ile au hata wakifungwa 1-0 itawafanya watinge hatua ya Makundi ya michuano hiyo.Wenger alisema: “Hii ni mechi muhimu kupita Jumamosi na Man U!! Ukifungwa leo hamna marudiano!! Tukifungwa Jumamosi na Man U bado tuna nafasi kwani tutabakiwa na mechi 35 za Ligi!!”Mbali ya ushindi wa uwanjani katika mechi ya leo, Timu ambazo zitacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huwa na uhakika wa kupata donge lisilopungua Pauni Milioni 25.Mechi ya leo itaanza saa 3 dakika 45 saa za bongo., ametamka mechi ya leo ya marudiano ya mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Timu yake Arsenal na Celtic itakayochezwa nyumbani kwa Arsenal Emirates Stadium ni mechi kubwa kupita mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England watakayocheza Old Trafford na Mabingwa Manchester United.Arsenal waliishinda Celtic mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0 na suluhu ya aina yeyote ile au hata wakifungwa 1-0 itawafanya watinge hatua ya Makundi ya michuano hiyo.Wenger alisema: “Hii ni mechi muhimu kupita Jumamosi na Man U!! Ukifungwa leo hamna marudiano!! Tukifungwa Jumamosi na Man U bado tuna nafasi kwani tutabakiwa na mechi 35 za Ligi!!”Mbali ya ushindi wa uwanjani katika mechi ya leo, Timu ambazo zitacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huwa na uhakika wa kupata donge lisilopungua Pauni Milioni 25.Mechi ya leo itaanza saa 3 dakika 45 saa za bongo.

Vurugu Carling Cup Uwanjani Upton Park: West Ham 3 Millwall 1

FA kuchunguza!!!FA, Chama cha Soka cha England, kimesema kitafanya uchunguzi juu ya vurugu zilizotokea ndani na nje ya Uwanja wa Uptown Park jana usiku ambako mtu mmoja alichomwa kisu katika mechi ya Timu mbili zote za mjini London zenye upinzani wa jadi West Ham na Millwall zilipokuwa zikicheza mechi ya mtoano ya Kombe la Carling.Timu hizi hazijawahi kukutana tangu Aprili 2005 kwa vile West Ham iko Ligi Kuu na Millwall inacheza Madaraja mawili chini yake yaani Ligi 2.Vurugu hizo zilianza nje ya uwanja kabla ya mechi pale mamia ya Mashabiki wasio na Tiketi ambao Polisi imesema walipanga kuleta fujo kuanza kurusha chupa, matofali na kuchoma moto.Ndani ya uwanja, West Ham wakiwa nyuma kwa bao 1 lililofungwa na Harris wa Millwall dakika ya 26, waliweza kusawazisha dakika ya 87 kupitia Junior Stanislas na kusababisha Mashabiki kuvamia uwanja wakishangilia.Katika dakika 30 za muda wa nyongeza, alikuwa Junior Stanislas tena alieifungia West Ham bao la pili kwa penalti na Mashabiki kwa mara ya pili wakavamia uwanja kushangilia.Hapo ndipo Refa akasimamisha mechi na kuwatoa nje Wachezaji huku Polisi na Wasimamizi wakijitahidi kuwaondoa Mashabiki uwanjani.Mmoja wa watu waliojitahidi kuwatuliza Washabiki ni Mchezaji wa West Ham Jack Collison ambae Baba yake Mzazi alifariki Jumapili kwa ajali ya pikipiki na ambae alisema licha ya msiba huo yuko tayari kucheza mechi hiyo.FA imesema Shabiki yeyote atakaegundulika kushiriki fujo hizo atafungiwa maisha kuingia kwenye Viwanja.

MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA CHAMPIONS LEAGUE [Kwenye mabano Timu inayosonga mbele na jumla ya magoli]Anderlect 1 v Lyon 3 [Lyon imeshinda jumla magoli 8-2]Atletico Madrid 2 v Panathinaikos 0 [Atletico 5-2]Debrecin 2 v Levski Sofia o [Debrecin 4-1]FC Zurich 2 v FK Ventspills 1 [FC Zurich 5-1]Maccabi Haifa 3 v SV Red Bull Salzburg 0 [Haifa 5-1]MECHI ZA LEO JUMATANO AGOSTI 26[Matokeo mechi ya kwanza kwenye mabano][saa 3 dak 45 usiku]Apoel Nicosia v FC Copenhagen [0-1]Arsenal v Celtic [2-0]Fiorentina v Sporting [2-2]Olympiacos v FC Sheriff Tiraspol [2-0]VfB Stuttgart v Politehnica Timisoara [2-0]

Monday, August 24, 2009

Lockerbie minister facing critics

Mr. MacAskill

The Scottish justice secretary will be forced to defend his decision to release the Lockerbie bomber as the Scottish Parliament is recalled.

Opposition parties will demand to know how Kenny MacAskill aims to repair the damage they claim has been done to Scotland's global reputation.

He has been under huge pressure after granting early release to terminally-ill Abdelbaset Ali al-Megrahi.

Mr MacAskill will make a statement to parliament and be questioned by MSPs.

The parliament will reconvene at 1430 BST on Monday.

Megrahi was freed after receiving a life sentence imposed in 2001 for his conviction for the UK's worst terrorist atrocity, which claimed 270 lives in 1988.

International standing

The 57-year-old, who has prostate cancer, returned home to Libya on Thursday to jubilant scenes which included people waving Scottish flags.

Scottish ministers said their decision to release Megrahi on compassionate grounds - which has been strongly criticised by the US government - followed due process and was the right one.

As the Scottish Parliament was preparing to cut short its summer break to discuss the issue, Scotland's opposition politicians urged Mr MacAskill to set out how he intends to improve Scotland's international standing in the wake of the criticism.

Greece braced for more fire chaos

Greek firefighters face another day battling wildfires that threaten areas north of Athens, as thousands leave their homes.

Moto mkubwa wateketeza Athens


Maelfu ya wakazi kadhaa wa mji wa Athens nchini Ugiriki wameokolewa katika nyumba zao kufuatia moto wa mstituni unaoendelea kuuzunguka mji mkuu huo.

Karibu watu wote wa Aglos Stefanos, kilomita 23 kutoka kaskazini mashariki mwa Athens, walikimbia moto huo kwa magari au kwa miguu.

Moto umekuwa ukiteketeza eneo la kilomita 50 ukichochewa kwa upepo mkali usiotabirika.

Moto huo ambao ni mkubwa kuliko ule wa mwaka 2007 uliouwa watu 70, unaelezewa kama ni angamizo kwa mazingira.

Juhudi za uzimaji moto zilisimamishwa wakati wa usiku giza lilipoanza kuingia siku ya Jumapili, huku moto huo ukiendelea kuwaka wakati wa usiku, ingawaje hakuna majeruhi walioripotiwa.

Ingawa moto huo umeripotiwa kupungua katika maeneo ya mjini ulikuwa bado unaendelea kuteketeza zaidi maeneo ya misitu.

''Kubadilikabadilika kwa mwelekeo wa upepo kunatabiri moto huo'' msemaji wa kikosi cha zama moto Giannis Kapakis ameliambia shirika la habari la Reuters. ''Ni lazima wote tuwe watulivu katika kipindi cha usiku huu.''

Nyumba kadhaa zimeteketezwa na hali ya hatari imetangazwa katika eneo la mji wa Athens.

Waziri mkuu Costas Karamanlis amesema nchi inakumbana na ''mkasa mzito'' lakini akapongeza juhudi za waokozi kwa juhudi zao za kishujaa.

Italia, Ufaransa na Cyprus zimetuma ndege kusaidiana na vikosi vya zima moto vya Ugiriki.

Polisi wakiwa na vipaza sauti walizunguka katika eneo la Agios Stefanos mapema Jumapili kuwaasa wakazi kuelekea Athens mara moja.

''Tumekuwa tukiomba serikali tangu asubuhi kutuma vikosi'', amesema Panayiotis Bitakos makamu Meya wa eneo hilo. ''Muda umekwisha sasa, umekwisha sana.''

Moto huo unaripotiwa kuwa umeanza siku ya Ijumaa katika eneo lililotengwa kutupa takataka la Grammatiko, karibu na mji mkongwe wa Marathon.

Moto huo unasambaa kwa kasi katika vilima nje ya mji wa Athens, ukiteketeza misitu.

Moto huo uliongezaka zaidi siku ya Jumamosi na kusambaa hadi Varnavas. Hadi siku ya Jumapili asubuhi nyumba zilikuwa zinaungua katika vitongoji vya Athens vya Drafi, Pikermi na Pallini.

Wakati wa usiku moto ulikumba kilele cha Pendeli, katika mwinuko, kitongoji cha kaskazini kinachoonyesha mandhari ya mji wa Athens, ukiteketeza majumba.

Sehemu kubwa ya mlima wa Pendeli iliteketezwa mwaka 2007, anasema Malcolm Brabant aliyeko Athens.

Miti iliyokuwa katika milima mitatu kati ya minne inayozunguka mjii mkuu Athens, ilishateketezwa katika matukio yaliyopita ya moto na mmomonyoko wa udongo katika misitu utakuwa ni wa kutisha, mwandishi wetu anaongeza.

Mkasa mzito

Mamia ya vikosi vya zima moto na wanajeshi vikisaidiwa kwa helikopta na ndege vimekuwa vikidondosha maji toka angani kuzima moto, lakini moto huo ulikuwa mkubwa kupindukia kuweza kudhibiti, mwandishi wetu anasema.

Gavana wa Athens Yiannis Sgouros ameiambia televisheni ya Ugiriki kuwa zaidi ya akari 30,000 za ardhi zimeteketezwa, katika kile anachokielezea kama ni ''maangamizi ya mazingira.''

Wakati wakazi wengi katika maeneo yaliyotishiwa na moto huo walifuata maelekezo ya kuhama, wengine walibaki wakijaribu kulinda nyumba zao.

Moto huo umesababisha moshi mzito katika anga la Athens.

Venezuela repeats at Miss Universe contest.

Dayana Mendoz

Miss Venezuela Stefania Fernandez, center, reacts as she is named Miss Universe 2009 next to Miss Universe 2008 Dayana Mendoza, also of Venezuela, right, at the end the Miss Universe beauty pageant in Nassau, Bahamas, Sunday, Aug. 23, 2009. Miss Dominican Republic Ada Aimee De la Cruz, left, was first runner up.

Sunday, August 23, 2009

Century man: Rooney afunga goli lake la 100 Man U walipomchapa mtu 5-0!!


Wayne Rooney amefunga goli lake la 100 akiwa na Man U kwenye mechi iliyowapa nguvu mpya, ari mpya na kelele mpwa mashabiki wa timu hiyo baada ya mwanzo mbaya na kufungwa na wiki iliyopita. Manchester United jana aliwafunga Wigan bila huruma bao 5-0 mabao ambayo yalifungwa kipindi cha pili.

Katika mchezo wa jana mabao wawili ya Rooney yalimuwezesha kuwa na magoli 101 katika timu ya Man U.

Owen ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa kupachka bao la kwanza kitokea benchi.

Dimitar Berbatov alifunga bao la pili na la mwisho lilifungwa na Nani.

Saturday, August 22, 2009

Liverpool wamsaini Mlinzi Kyrgiakos.

Klabu ya Liverpool imekamilisha taratibu za kumsaini Beki wa Kimataifa wa Ugiriki Sotirios Kyrgiakos kutoka AEK Athens kwa ada ya Pauni Milioni 2.Kyrgiakos, miaka 30, anaecheza kama Sentahafu, aliwahi kuichezea Rangers ya Scotland na amesaini mkataba wa miaka miwili.Wakati huohuo, Beki wa Liverpool, Daniel Agger, atafanyiwa upasuaji wa mgongo na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6.Adriano arudishwa tena Timu ya BrazilMshambuliaji Adriano alieisusa Inter Milan na kugoma kurudi kwenye Timu hiyo na sasa yuko kwao Brazil akichezea Klabu ya Flamengo, ameitwa tena kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachocheza na Wapinzani wao wakubwa Argentina Septemba 5 kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia. Siku 4 baadae Brazil watachuana na Chile kwenye mashindano hayo hayo.Kikosi kamili:Makipa: Julio Cesar (Inter Milan), Victor (Gremio);Walinzi: Andre Santos (Fenerbahce), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (Inter), Filipe (Deportivo La Coruna), Lucio (Inter), Luisao (Benfica), Miranda (Sao Paulo), Juan (AS Roma);Viungo: Elano (Galatasaray), Felipe Melo (Juventus), Gilberto Silva (Panathinaikos), Josue (VfL Wolfsburg), Ramires (Benfica), Julio Baptista (AS Roma), Kaka (Real Madrid), Lucas (Liverpool);Washambuliaji: Luis Fabiano (Sevilla), Nilmar (Villarreal), Robinho (Manchester City), Adriano (Flamengo)

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndo umeanza, blog hii yapenda kuwatakia mfungo mwema wa mwezi huu mtukufu na pia kuwaasa wale wote wanaofunga kuwa kufuata mafundisho ya Quran Tukufu kuhusu mwezi huu. Tunasema Ramadan Kareem.wa Ramadhani ndo umeanza, blog hii yapenda kuwatakia mfungo mwema wa mwezi huu mtukufu na pia kuwaasa wale wote wanaofunga kuwa kufuata mafundisho ya Quran Tukufu kuhusu mwezi huu. Tunasema Ramadan Kareem.

Friday, August 21, 2009

EUROPA LEAGUE

EUROPA LEAGUE: Everton na Fulham zapeta mechi ya kwanza nyumbani, Villa yapigwa kimoja ugenini!!!
Kwenye mechi za kwanza za mchujo wa kuwania kuingia kwenye Makundi ya EUROPA LEAGUE Klabu za England Aston Villa, Everton na Fulham, zilizomaliza LIGI KUU England zikiwa nafasi za 5, 6 na 7 na hivyo kupata nafasi kucheza Ulaya, leo zilitupa karata zao na ni Aston Villa pekee waliocheza ugenini walifungwa bao 1-0 na Rapid Vienna ya Austria huku Everton na Fulham zikipata ushindi mnono kwao.
Everton waliibamiza Sigma Olomouc ya Urusi kwa mabao 4-0 mawili mguuni kwa Luis Saha na mengine mawili toka kwa Chipukizi Jack Rodwell.
Fulham waliinyuka Amkar Perm ya Urusi 3-1 kwa mabao ya Jonhson, Dempsey na Zamora.
Marudiano ya mechi hizi ni wiki ijayo.
Matokeo mengine ni:
Ajax 2 Bratislava 0
CSKA Sofia 0 Dinamo Moscow 0
FC Twente 3 FK Qabarag 1
Guingamp 1 Hamburg 5
MFK Kosice 3 Roma 3.

EUROPA LEAGUE

EUROPA LEAGUE: Everton na Fulham zapeta mechi ya kwanza nyumbani, Villa yapigwa kimoja ugenini!!!
Kwenye mechi za kwanza za mchujo wa kuwania kuingia kwenye Makundi ya EUROPA LEAGUE Klabu za England Aston Villa, Everton na Fulham, zilizomaliza LIGI KUU England zikiwa nafasi za 5, 6 na 7 na hivyo kupata nafasi kucheza Ulaya, leo zilitupa karata zao na ni Aston Villa pekee waliocheza ugenini walifungwa bao 1-0 na Rapid Vienna ya Austria huku Everton na Fulham zikipata ushindi mnono kwao.
Everton waliibamiza Sigma Olomouc ya Urusi kwa mabao 4-0 mawili mguuni kwa Luis Saha na mengine mawili toka kwa Chipukizi Jack Rodwell.
Fulham waliinyuka Amkar Perm ya Urusi 3-1 kwa mabao ya Jonhson, Dempsey na Zamora.
Marudiano ya mechi hizi ni wiki ijayo.
Matokeo mengine ni:
Ajax 2 Bratislava 0
CSKA Sofia 0 Dinamo Moscow 0
FC Twente 3 FK Qabarag 1
Guingamp 1 Hamburg 5
MFK Kosice 3 Roma 3

Lampard: "Ni Messi tu anaweza kumbadili Ronaldo!"

Kiungo wa Chelsea Franck Lampard amesema Manchester United hawawezi kupata mbadala wa Cristiano Ronalndo labda wamchukue Messi.
Hata hivyo Lampard amesema anaamini pengo la Ronaldo litazibwa kwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kuifanya Timu hiyo icheze "kitimu" badala ya kutegemea mtu mmoja na hivyo amekiri Man U itakuwa tishio.
Rio nje mwezi!!
Taarifa zinasema Beki kigogo wa Manchester United, Rio Ferdinand, atakuwa nje ya uwanja mwezi mzima baada ya kuumia musuli pajani mazoezini.
Hivyo Ferdinand ataikosa mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Wigan na Jumamosi ijayo dhidi ya Arsenal.

Thursday, August 20, 2009

Nelson Mandela Bay ready for 2010!!

In the city's colourful promotional brochure, Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth boasts of being the "best tourist destination" in South Africa. After a short tour around the city, it is not hard to see why such a bold claim has emblazoned across the booklet's front cover.
Situated in the Eastern Cape Province, where some of the country's most celebrated figures hail from, there are many compelling reasons why Nelson Mandela Bay/ Port Elizabeth should be an essential stop for tourists during next year's FIFA World Cup.
"We believe the Nelson Mandela Bay will be one of the biggest tourist attractions during the World Cup," Nelson Mandela Bay spokesperson, Roland Williams told FIFA.com. "Our goal is to market and position the city as a destination of choice far beyond 2010. We have worked very hard and one can see that our infrastructure is one of the best in the country."
The warm beaches, the wildlife, the breathtaking views and the natural vegetation on view as you drive through this vast province go towards making a trip to the south-eastern part of the country a must. The Eastern Cape is home to Nelson Mandela, an iconic figure in South Africa and throughout the world. It has also given birth to the likes of another former South African president, Thabo Mbeki, as well as Steve Biko, the architect of Black Consciousness in South Africa, Govan Mbeki, Oliver Tambo, Walter Sisulu and many others.
Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth is also the birthplace of Blackburn Rovers and Bafana Bafana winger, Elrio van Heerden. Currently, the city does not have a top flight outfit following the sudden relegation of Bay United from the elite league last season. However, some of the country's major teams continue to use the city for matches.
Recently, Nelson Mandela Bay launched three Visitor Information Centres (VICs) to ensure tourists arriving in the city for the 2010 FIFA World Cup™ receive the best advice and information. The three centres are based at the Port Elizabeth Airport, the lighthouse facility at the Donkin Reserve and the Boardwalk Casino and Entertainment World. These one-stop shops will supply tourists with information on a wide range of services, including reservations, accommodation, tours, vehicle hire, entertainment, adventure and travel tips. Visitors to the centre will also be able to make use of user-friendly touch screens linked to central database of tourism products on offer and the advertisements of local businesses.
New StadiumTwo months after its completion, the state-of-the-art Nelson Mandela Bay Stadium has already passed two major tests in its quest to be ready for the FIFA World Cup.
The stadium achieved a milestone when it became the first newly-built South Africa 2010 venue to be completed - a full 12 months before the world's greatest showpiece descends on the African continent for the first time ever.
The Nelson Mandela Bay Stadium recently hosted two major events: the British Lions Tour and the country's biggest football encounter popularly known as the Soweto Derby between historical arch-rivals Orlando Pirates and Kaizer Chiefs.
"It is clear for everyone to see that the Nelson Mandela Bay is ready," Williams added. "We managed to complete our stadium more than a year before the event; that on its own should say something to those who still believe we won't be able to successfully host this event."
The Nelson Mandela Bay Stadium will host group games during the 64-match event next year. The stadium will also be the venue for the third and fourth place play.