Friday, August 28, 2009

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUEKlabu 5 za Uingereza zimewekwa kwenye Makundi ambayo Wadau wengi wamedai ni “laini kidogo” baada ya kuepuka kupangwa na Timu Vigogo wa Ulaya. Manchester United ambao walifika Fainali msimu uliopita wapo pamoja na CSKA Moscow, Besiktas na Wolfsburg KUNDI B.Liverpool watamenyana na Lyon, Fiorentina na Debrecen wakati Chelsea wapo na Porto, Atletico Madrid na APOEL Nicosia.Arsenal wamepangiwa na AZ Alkmaar, Olympiakos na Standard Liege wakati Rangers ya Scotland itacheza na Stuttgart, Sevilla na Unirea Urziceni.Klabu za England zimekwepa kuwekwa na Real Madrid na Inter Milan huku Real akiwa Kundi moja na AC Milan, Marseille na FC Zurich.Inter Milan yuko pamoja na Barcelona, Dynamo Kiev na Rubin Kazan.Msimu uliokwisha Chelsea walitolewa nje na Brcelona kwenye Nusu Fainali kwa bao la Andres Iniesta la dakika za majeruhi na Mkurugenzi Mtendaji wao Peter Kenyon alizungumza baada ya upangaji Makundi na kusema: “Tunaanza upya na siku zote tunataka twende mbele zaidi. Hamna mechi rahisi au Kundi laini lakini tumewakwepa Vigogo!!”Manchester United, kwa kuwa Kundi moja na CSKA Moscow, watarudi tena Uwanja wa Luzhniki walipowatoa Chelsea Fainali ya 2008 na kuwa Bingwa wa Ulaya na Mkuurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo David Gill ametamka: “Kwa ujumla, tunafurahia Kundi letu. Tuna shauku kubwa kurudi tena Moscow baada ya furaha ya 2008!”Lakini, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alisema: “CSKA sasa wamejijenga sana na mechi za kuchezea Uturuki ni ngumu siku zote. Pia tunajua ubora wa Wolfsburg na mafanikio yao Bundesliga msimu uliopita.”Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Liverpool, Christian Purslow, amesema: “Tumefurahia!”Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alionyesha tahadhari kuhusu KUNDI H ambalo wao wapo na kutamka: “Wengine wataangalia na kusema Arsenal atapita lakini tupo makini. Itakuwa ngumu ila tutatimiza kazi yetu.”Yapo Makundi Manane yenye Timu 4 kila moja na mechi zitachezwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 15 na 16.Washindi wanane wa kila Kundi pamoja na Washindi wa pili wataingia hatua ya mtoano huku washindi wa tatu wakiingizwa EUROPA LIGI.Fainali itachezwa Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium tarehe 22 May 2010 ambayo ni Jumamosi tofauti na hapo nyuma Fainali kuchezwa Jumatano.

No comments:

Post a Comment