Friday, August 28, 2009

Villa nje, Fulham, Everton wapeta EUROPA LIGI!!!

Licha ya kufungwa ugenini bao 1-0 na Amkar Perm ya Urusi, Fulham imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI kwa jumla ya mabao 3-2 huku wenzao Everton wakijumuika nao baada ya pia kuwa ugenini na kutoka suluhu ya 1-1 na Sigma Olomouc ya Czech Republic na kutinga kwenye Makundi kwa jumla ya mabao 5-1.Kwa Aston Villa, licha ya kushinda uwanjani kwao 2-1 dhidi ya Rapid Vienna ya Austria, Villa imebwagwa nje ya EUROPA LIGI kwa bao la ugenini kwani ilifungwa mechi ya kwanza bao 1-0 na hivyo jumla ya mabao kuwa 2-2 katika mechi mbili.Droo ya kuamua Timu zipi zitakuwa Kundi lipi itafanywa leo huko Monaco kabla ya mechi ya leo kugombea SUPER CUP kati ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Barcelona, na Bingwa wa UEFA CUP, Shakhtar Donetsk.

No comments:

Post a Comment