Saturday, August 22, 2009

Liverpool wamsaini Mlinzi Kyrgiakos.

Klabu ya Liverpool imekamilisha taratibu za kumsaini Beki wa Kimataifa wa Ugiriki Sotirios Kyrgiakos kutoka AEK Athens kwa ada ya Pauni Milioni 2.Kyrgiakos, miaka 30, anaecheza kama Sentahafu, aliwahi kuichezea Rangers ya Scotland na amesaini mkataba wa miaka miwili.Wakati huohuo, Beki wa Liverpool, Daniel Agger, atafanyiwa upasuaji wa mgongo na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 6.Adriano arudishwa tena Timu ya BrazilMshambuliaji Adriano alieisusa Inter Milan na kugoma kurudi kwenye Timu hiyo na sasa yuko kwao Brazil akichezea Klabu ya Flamengo, ameitwa tena kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachocheza na Wapinzani wao wakubwa Argentina Septemba 5 kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia. Siku 4 baadae Brazil watachuana na Chile kwenye mashindano hayo hayo.Kikosi kamili:Makipa: Julio Cesar (Inter Milan), Victor (Gremio);Walinzi: Andre Santos (Fenerbahce), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (Inter), Filipe (Deportivo La Coruna), Lucio (Inter), Luisao (Benfica), Miranda (Sao Paulo), Juan (AS Roma);Viungo: Elano (Galatasaray), Felipe Melo (Juventus), Gilberto Silva (Panathinaikos), Josue (VfL Wolfsburg), Ramires (Benfica), Julio Baptista (AS Roma), Kaka (Real Madrid), Lucas (Liverpool);Washambuliaji: Luis Fabiano (Sevilla), Nilmar (Villarreal), Robinho (Manchester City), Adriano (Flamengo)

No comments:

Post a Comment