Sunday, August 9, 2009

Milioni wakimbia tufani Uchina

Serikali nchini China imewahamisha wakazi takribani milioni moja wanaoishi katika pwani ya kusini mashariki mwa Uchina katika kuepuka tufani inayojulikana kama Morakot.

Jumla ya wakazi 473,000 wa jimbo la Zhejiang wamehamishwa, ikiwa ni pamoja na wakazi 480,000 kutoka wilaya ya Fujian, Xinhua.

Zaidi ya mashua 35,000 zimepelekwa katika maeneo ya mwambao. Tufani ya Morakot imesababisha mvua kubwa ya ujazo wa milimita 2.5 katika kisiwa chaTaiwan.

Mafuriko ya Taiwan yamekuwa ni makubwa kabisa kutokea katika mikoa ya kusini katika kipindi cha nusu karne.

Kimbunga cha Morakat pia kimesababisha mvua kubwa maeneo ya Philippines ambapo kwa uchache watu 10 waliuawa katika mafuriko na maporomoko katika maeneo ya kaskazini.

Serikali za majimbo zimetuma zaidi ya ujumbe wa simu milioni 8 kwa wakazi ikiwaatahadharisha kukaribia kwa kimbunga hicho, shirika la habari la serikali ya Uchina linaarifu.

Kutokea kwa tufani ni jambo ya kawaida katika eneo hilo hususani katika kipindi cha mwezi wa saba na wa tisa.

Kisiwani Taiwan mvua kubwa ya ujazo wa sentimita 200 ilinyesha siku ya Ijumaa na Jumamosi peke yake, kwa mujibu wa Mamlaka Kuu ya Hali ya Hewa ya eneo hilo.

Kwa uchache watu 29 waliripotiwa kupotea na mmoja kufa baada ya tufani hiyo kukikumba kisiwa hicho.

Taarifa zinasema kuwa mafuriko hayo yalibomoa nyumba kusini mwa Kaohsiung na kusababisha watu 16 kupotea.

Watu wengine watatu walichukuliwa na maji kusini mashariki mwa mkoa wa Taitung, wawili kati yao wakiwa ni askari polisi waliokuwa wakisaidia kuwahamisha wanavijiji.

Hoteli moja kusini mwa kisiwa hicho ilianguka baada ya mafuriko hayo kuchimba na kuharibu kabisa msingi wa jengo la hoteli hiyo.

Inaaminika kuwa watu waliokuwemo katika hoteli hiyo walikuwa tayari wameshahamishwa kabla ya kutokea kwa maafa hayo.

Serikali nchini china imewahamisha wakazi takribani milioni moja wanaoishi katika pwani ya kusini mashariki mwa China katika kuepuka tufani inayojulika kama Morakot.

Jumla ya wakazi 473,000 wa jimbo la Zhejiang wamehamishwa ikiwa ni pamoja na wakazi 480,000 kutoka wilaya ya Fujian, Xinhua.

Zaidi ya mashua 35,000 zimepelekwa ufukweni. Tufani ya Morakot imesababissha mvua kubwa ya ujazo wa milimita 2.5 katika kisiwa chaTaiwan.

Mafuriko ya Taiwan yamekuwa ni ya hatari sana kutokea katika mikoa ya kusini tokea kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Morakat pia imesababisha mvua kubwa nchini Philippines ambapo kwa uchache watu 10 waliuawa katika mafuriko na maporomoko katika maeneo ya kaskazini.

Serikali za majimbo zimetuma zaidi ya ujumbe wa simu milioni 8 kwa wakazi ikiwaatahadharisha kukaribia kwa tufani, shirika la habari la serikali ya China linaarifu.

Tufani ni matukio ya kawaida katika eneo hilo hususani katika kipindi cha mwezi wa saba na wa tisa.

Huko Taiwan mvua kubwa ya ujazo wa sentimita 200 ilinyesha siku ya Ijumaa na Jumamosi peke yake, kwa mujibu wa Mamlaka Kuu ya Hali ya Hewa ya eneo hilo.

Kwa uchache watu 29 waliripotiwa kupotea na mmoja kufa baada ya tufani hiyo kukumba kisiwa hicho.

Taarifa zinasema kuwa mafuriko hayo yalibomoa nyumba kusini mwa Kaohsiung
na kusababisha watu 16 kupotea.

Watu wengine watatu walichukuliwa na maji kusini mashariki mwa mkoa wa Taitung wawili kati yao wakiwa ni askari polisi waliokuwa wakisaidia kuwahamisha wanavijiji.

Hoteli moja kusini mwa kisiwa hicho ilianguka baada ya mafuriko hayo kuchimba na kuharibu kabisa msingi wa jengo la hoteli hiyo.

Inaaminika kuwa watu waliokuwemo katika hoteli hiyo walikuwa tayari wameshahamishwa kabla ya kutokea kwa maafa hayo.

Hoteli hiyo katika eneo la Chihpen ni moja kati ya hoteli maarufu zinazojulikana sana Taiwan.

Milioni wakimbia tufani Uchina

No comments:

Post a Comment