Friday, August 28, 2009

UHAMISHO LIGI KUU ENGLAND!!!!!

Zikiwa zimebaki siku chache kabla dirisha la uhamisho halijafungwa hapo Agosti 31, spidi ya uhamisho imepamba moto huku Klabu nyingi bado zikichacharika kusaka Wachezaji.Baadhi ya biashara zilizokamilika hivi karibuni ni pamoja na uhamisho wa Mlinzi na Nahodha wa Manchester City Richard Dunne, miaka 29, kuhamia Aston Villa.Aston Villa pia imemchukua Stephen Warnock, miaka 27,kutoka Blackburn Rovers kwa mkataba wa miaka minne.Warnock, anaeweza kucheza kama Kiungo au Beki wa kushoto, alijiunga na Blackburn mwaka 2007 akitokea Liverpool.Mlinzi wa Portsmouth Sylvain Distin, miaka 31, amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitatu na ada ambayo haikutajwa.Nao Wachezaji wa Middlesbrough iliyoshushwa Daraja msimu uliokwisha, Robert Huth, mlinzi kutoka Ujerumani na Tuncay Sanli wa Uturuki, wamejiunga na Stoke City.Blackburn Rovers wamemsaini Pascal Chimbonda kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Tottenham Hotspur.

No comments:

Post a Comment