Thursday, August 6, 2009

Rais Zuma, atangaza mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi


Rais wa Afrika kusini , Jacob Zuma, ametangaza mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi, kwa lengo la kuwasaidia wafanyakazi wanaokabiliwa na tisho la kufutwa kazi. Mpango huo utagharimu jumla ya dola milioni mia tatu.

Bwana Zuma amesema pesa hizo zitatumika kwa mpango huo wa miezi mitatu kutoa mafunzo hususan kwa wafanyakazi wenye kipato cha chini

Hatua hii huenda ikasababisha makampuni makubwa angalau kuwaacha wafanyakazi kuhudhuiria mafunzo hayo badala ya kuwafuta kazi kabisa.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoendelea ulimwenguni zenye idadi kubwa ya watu wasiokuwa na ajira. Nchini humo mtu mmoja kati ya wanne ambao wamefika umri wa kufanya kazi hana ajira. Idadi kubwa ya watu nchini humo wana ujuzi wa kiwango cha chini.

Mpango huu mpya unanuia kuimarishi umahiri wa wafanyi kazi unaohitajika katika maisha ya kisasa, kama vile teknolojia ya mawasiliano, kumaliza ujinga na kuwaelimisha kuhusu tarakimu.

Jacob Zuma ameahidi mara kwa mara kuwa anataka kupunguza idadi ya watu wasiokuwa na ajira. Ameahidi kuanzisha nafasi nusu millioni za kazi kufikia mwisho wa mwaka huu na kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasiokuwa na ajira kabla ya mwaka wa 2014.

Mwezi uliopita raia wa nchi hiyo waliandamana katika miji mbali mbali nchini humo wakilalamikia kile walichokiona kama kushindwa kwa serikali kuwapa huduma muhimu za afya, kuwapa ajira na makazi ya kutosha.

No comments:

Post a Comment