Wednesday, August 26, 2009

Wenger: “Leo na Celtic ni Mechi Kubwa kupita Jumamosi na Man U!!!”

Meneja wa Arsenal,Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametamka mechi ya leo ya marudiano ya mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Timu yake Arsenal na Celtic itakayochezwa nyumbani kwa Arsenal Emirates Stadium ni mechi kubwa kupita mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England watakayocheza Old Trafford na Mabingwa Manchester United.Arsenal waliishinda Celtic mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0 na suluhu ya aina yeyote ile au hata wakifungwa 1-0 itawafanya watinge hatua ya Makundi ya michuano hiyo.Wenger alisema: “Hii ni mechi muhimu kupita Jumamosi na Man U!! Ukifungwa leo hamna marudiano!! Tukifungwa Jumamosi na Man U bado tuna nafasi kwani tutabakiwa na mechi 35 za Ligi!!”Mbali ya ushindi wa uwanjani katika mechi ya leo, Timu ambazo zitacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huwa na uhakika wa kupata donge lisilopungua Pauni Milioni 25.Mechi ya leo itaanza saa 3 dakika 45 saa za bongo., ametamka mechi ya leo ya marudiano ya mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Timu yake Arsenal na Celtic itakayochezwa nyumbani kwa Arsenal Emirates Stadium ni mechi kubwa kupita mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England watakayocheza Old Trafford na Mabingwa Manchester United.Arsenal waliishinda Celtic mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0 na suluhu ya aina yeyote ile au hata wakifungwa 1-0 itawafanya watinge hatua ya Makundi ya michuano hiyo.Wenger alisema: “Hii ni mechi muhimu kupita Jumamosi na Man U!! Ukifungwa leo hamna marudiano!! Tukifungwa Jumamosi na Man U bado tuna nafasi kwani tutabakiwa na mechi 35 za Ligi!!”Mbali ya ushindi wa uwanjani katika mechi ya leo, Timu ambazo zitacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huwa na uhakika wa kupata donge lisilopungua Pauni Milioni 25.Mechi ya leo itaanza saa 3 dakika 45 saa za bongo.

No comments:

Post a Comment