Wednesday, August 19, 2009

-Kipa wa zamani wa Arsenal kustaafu soka!!!
Jens Lehman, Kipa wa zamani wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Ujerumani, ambae atafikisha umri wa miaka 40 Novemba mwaka huu, atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu ulioanza majuzi.
Lehman, ambae kwa sasa ni Kipa wa Klabu iliyo Bundesliga VfB Stuttgart, ameidakia Timu ya Ujerumani mara 61 na kucheza Arsenal kati ya 2003 na 2008.
-Wakala wa Vidic akanusha Nemanja kwenda Barca!!!
Paolo Fabbri, Wakala wa Beki mahiri wa Mabingwa Manchester United, Nemanja Vidic, amekanusha taarifa zilizomnukuu yeye na kuzagaa sana leo hii kuwa ametamka Vidic ana nia ya kuhamia Spain Klabuni Barcelona.
Fabbri amesema yeye hakusema hayo ila anachojua ni kuwa Vidic anajisikia raha kuwa na Manchester United.

No comments:

Post a Comment