Sunday, August 23, 2009

Century man: Rooney afunga goli lake la 100 Man U walipomchapa mtu 5-0!!


Wayne Rooney amefunga goli lake la 100 akiwa na Man U kwenye mechi iliyowapa nguvu mpya, ari mpya na kelele mpwa mashabiki wa timu hiyo baada ya mwanzo mbaya na kufungwa na wiki iliyopita. Manchester United jana aliwafunga Wigan bila huruma bao 5-0 mabao ambayo yalifungwa kipindi cha pili.

Katika mchezo wa jana mabao wawili ya Rooney yalimuwezesha kuwa na magoli 101 katika timu ya Man U.

Owen ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa kupachka bao la kwanza kitokea benchi.

Dimitar Berbatov alifunga bao la pili na la mwisho lilifungwa na Nani.

No comments:

Post a Comment